99. Az-Zalzala
1Itakapotikiswa ardhi mtikiso wa nguvu
2Na ikatoa vilivyomo ndani yake: wafu na makandi
3Na akauliza binadamu, kwa babaiko, «Imezukiwa na nini?»
4Siku ya Kiyama ardhi itatoa habari ya mambo iliyofanyiwa ya uzuri na ubaya
5kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kutukuka, Ameiamuru itoe habari ya mambo iliyofanyiwa
6Siku hiyo wataondoka kutoka kwenye kisimamo cha Hesabu wakiwa makundi, ili Mwenyezi Mungu Awaoneshe waliyoyatenda, mazuri na mabaya, na Awalipe kwayo
7Yoyote mwenye kufanya jema wezani wa chungu mdogo atayaona malipo yake Akhera
8Na yoyote mwenye kufanya baya wezani wa chungu mdogo atayaona malipo yake Akhera
chanzo: Abdullah Muhammad Abu Bakr
WEBREATH · 11:11
«If you are thankful, I will give you more» — Quran 14:7
Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.
WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath