98. Al-Bayyina
1Hawakuwa wenye kukufuru miongoni mwa Mayhudi na Wanaswara na washirikina ni wenye kuacha ukafiri wao mpaka uwajilie wao ushahidi walioahidiwa katika vitabu vilivyopita
2Nao ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, Muhammad , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, atakayewasomea Qur’ani iliyomo kwenye kurasa safi
3Ndani ya kurasa hizo mna habari za kweli na amri za uadilifu zenye kuongoza kwenye haki na kwenye njia ilionyoka
4Na hawakutofautiana wale waliopewa Kitabu, miongoni mwa Mayahudi na Wanaswara, juu ya kuwa Muhammad , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, ni Mtume wa kweli, kwa sifa zake waliokuwa wakiziona katika vtabu vyao isipokuwa baada ya kuwathibitikia kuwa yeye ndiye Nabii waliyoahidiwa katika Taurati na Injili. Walikuwa wanakubali , kwa umoja wao, kuwa unabii wake ni wa kweli. Lakini alipotumilizwa waliukanusha na wakatofautiana
5Na hawakuamrishwa katika sheria zote zilizopita isipokuwa ni wamuabudu Mwenyezi Mungu Peke Yake, wakikusudia kwa ibada yao kupata Radhi Zake, hali ya kuepuka upande wa ushirikina na kuelekea kwenye Imani, wasimamishe Swala na watoe Zaka. Kufanya hayo ndio Dini iliyolingana , nayo ni Uislamu
6Hakika wale waliokufuru miongoni mwa Mayahudi na Wanaswara na Washirikina, mateso yao ni Moto wa Jahanamu. Watakuwa ni wenye kukaa milele humo. Wao ndio viumbe waovu kabisa
7Hakika wale waliomuamini Mwenyezi Mungu, wakamfuata Mtume wake na wakafanya amali njema, wao ndio bora wa viumbe
8Malipo yao , mbele ya Mola wao Siku ya Kiyama, ni Pepo ya makazi na utulivu yenye upeo wa uzuri, ambayo chini ya majumba yake ya fahari inapita mito; watakaa milele humo. Mwenyezi Mungu Ameridhika nao Akakubali amali zao njema. Na wao wameridhika na Yeye kwa maandalio Aliyowafanyia ya aina mbalimbali za takrima. Malipo mazuri hayo ni ya aliyemuogopa Mweyezi Mungu na akajiepusha na maasia
chanzo: Abdullah Muhammad Abu Bakr
WEBREATH · 11:11
«If you are thankful, I will give you more» — Quran 14:7
Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.
WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath