96. Al-Alaq
1Soma, ewe Nabii, Qur’ani uliyoteremshiwa ukianza kwa Jina la Mola wako Aliyepwekeka kwa kuumba
2Aliyemuumba kila binadamu kwa pande la damu nzito nyekundu
3Soma, ewe Nabii, kile ulichoteremshiwa, na Mola wako ni Mwingi wa wema, Mwingi wa ukarimu
4Aliyewafundisha viumbe vyake kuandika kwa kalamu
5Alimfundisha binadamu vitu ambavyo hakuwa akivijua. Akamtoa kwenye giza la ujinga, Akampeleka kwenye nuru ya elimu
6Kweli, binadamu hukiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu
7akijiona ametosheka kwa utajiri wake
8Basi, ajue kila mwenye kutupa mipaka kuwa mwisho atarudi kwa Mwenyezi Mungu Ambaye Atamlipa kila binadamu kwa alilolitenda
9Je, umeona ujeuri wa ajabu zaidi kuliko wa mtu huyu, Abu jahl
10Anayemkataza mja wetu, Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, anapomsalia Mola wake
11Waonaje iwapo mwenye kukatazwa kusali yuko uongofuni, vipi anamkataza
12Au iwapo anaamrisha mwigine kumcha Mungu, vipi anamkataza hilo
13Waonaje iwapo huyu mwenye kukataza anakanusha lile alinganiwalo kwalo na kulipa mgongo
14hajui kuwa Mwenyezi Mungu anaona kila analolifanya
15Basi mambo si kama anvyodai Abu Jahl. Na asipokomeka na ushindani alionao na udhia wake, Tutamshika upaa wake kwa nguvu na kumtia Motoni
16Upaa wake ni upaa wenye maneno ya urongo na vitendo vya makosa
17Basi na awalete, mtupaji mipaka huyu, watu wa baraza ili wamsaidiye
18Sisi Tutawaita Malaika wa adhabu
19Mambo si kama Abu Jahl anavyoyadhania. Yeye, ewe Mtume, hawezi kukufanya lolote la kukudhuru Usimfuate kwa lile alilokuitia la kuwa uache Swala, bali msujudie Mola wako na uwe karibu na Yeye kwa kujipendekeza Kwake kwa kumtii
chanzo: Abdullah Muhammad Abu Bakr
WEBREATH · 11:11
«If you are thankful, I will give you more» — Quran 14:7
Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.
WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath