94. Ash-Sharh
1Kwani Hatukukunjulia, ewe Mtume, kifua chako kwa sheria za Dini, kulingania watu kwa Mwenyezi Mungu na kujipamba kwa tabia nzuri
2Tukakuondolea mazito yako yaliyoemea mgongo wako
3na Tukakuweka, kwa matukufu Tuliyokuneemesha
4kwenye cheo cha juu
5Usirudi nyuma katika kueneza ujumbe uliotumwa nao kwa makero ya maadui zako. Kwani kwenye dhiki kuna faraji
6Hakika kwenye dhiki kuna faraji
7Basi utakapomaliza mambo ya kidunia na shughuli zake jipinde kwa kufanya ibada
8Na kwa Mola wako Peke Yake weka matumaini yako
chanzo: Abdullah Muhammad Abu Bakr
WEBREATH · 11:11
«If you are thankful, I will give you more» — Quran 14:7
Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.
WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath