Uislamu
nyuma

93. Ad-Dhuhaa

1Mwenyezi Mungu Anaapa kwa wakati wa dhuha, na uliokusudiwa ni wakati wa mchana mzima

2Na kwa usiku utuliapo na viumbe na likashadidi giza lake. Mwenyezi Mungu Huapa kwa Atakacho katika viumbe vyake. Ama kiumbe, hafai kuapa kwa asiyekuwa Muumba wake. Kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni ushirikina

3Hakukuwacha Mola wako, ewe Mtume, wala Hakukuchukia kwa kuchelewesha kukuteremshiaWahyi

4Na Nyumba ya Akhera ni bora kwako kuliko nyumba ya ulimwengu

5Na Atakupa Mola wako, ewe Mtume, neema ya kila sampuli uridhike

6Kwani Hakukupata, kabla ya hapo, kuwa ni yatima Akakukusanya na kukutunza

7Na Akakupata hujui Kitabu wala Imani, Akakufundisha yale amabayo ulikuwa huyajui na akakuafikia kufanya amali bora

8Na Akakupata masikini, Akakuletea riziki yako na Akakutajirisha kwa kutosheka na kusubiri

9Basi yatima usimtende ubaya

10Na muombaji usimkaripie, bali mlishe na umtimizie haja yake

11Na ama neema ya Mola wako Aliyokuneemesha nayo izungumze

chanzo: Abdullah Muhammad Abu Bakr

WEBREATH · 11:11

«If you are thankful, I will give you more» — Quran 14:7

Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.

WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath