Uislamu
nyuma

92. Al-Lail

1Mwenyezi Mungu Anaapa kwa usiku unapoifinika ardhi na vilivyoko juu yake kwa giza lake

2Na kwa mchana unapofunuka mwangaza wake kutoka kwenye giza la usiku

3Na kwa kuumba mbea mbili: ya kiume na ya kike

4Kuwa vitendo vyenu vinatofautiana: kuna wenye kufanyia dunia na wenye kufanyia Akhera

5Ama mwenye kutoa kwenye mali yake, akamcha Mwenyezi Mungu katika huko kutoa

6akaamini «Lā Ilāha Illā Allāh» na yanayotakiwa na Imani hiyo na akaamini malipo yanayofungamana nayo

7Tutamuongoza na kumuafikia njia za kheri na wema na kumsahilishia mambo yake

8Na ama mwenye kuyafanyia ubakhili mali yake, asiwe na haja ya malipo ya Mola wake

9akakanusha neno la «Lā Ilāha Illā Allāh» na yanayotakiwa na neno hilo na akakanusha malipo yanayofungamana nalo

10Tutamnyoshea njia za mateso

11Wala hayatamfaa yeye mali yake aliyoyafanyia ubakhili atakapotumbukia Motoni

12Ni juu Yetu, kwa fadhila Zetu na busara Yetu, kueleza njia ya uongofu yenye kufikisha kwa Mwenyezi Mungu na ya upotevu

13Na Sisi Tuna mamlaka ya maisha ya Akhera na maisha ya ulimwenguni

14Ndipo nikawaonya , enyi watu, na kuwatisha moto wenye kuwaka, nao ni moto wa Jahanamu

15Hataingia Moto huo isipokuwa aliyekuwa mbaya sana. Mwenye kumkanusha Nabii Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie

16na akakataa kumwamini na kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake

17Na ataepushwa nao mchaji Mwenyezi Mungu sana

18Ambaye hutoa mali yake kwa kutaka nyongeza za kheri

19kutoa Kwake si kwa kulipa zema alizofanyiwa na mtu

20Lakini anatoa kwa kutaka uso wa Mola wake na radhi zake. Basi Mwenyezi Mungu atampa

21huko Peponi, malipo ya kumridhisha

chanzo: Abdullah Muhammad Abu Bakr

WEBREATH · 11:11

«If you are thankful, I will give you more» — Quran 14:7

Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.

WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath