Uislamu
nyuma

91. Ash-Shams

1Mwenyezi Mungu Anaapa kwa jua na mchana wake na mwangaza wake wa asubuhi

2Na kwa mwezi unapolifuata wakati wa kucha na kutwa

3Na kwa mchana unapoliondoa giza na kulifunua

4Na kwa usiku unapoifinika ardhi ikawa giza

5Na kwa mbingu na kujengeka kwake kiimara

6Na kwa ardhi na kutandikika kwake

7Na kwa kila nafsi na namna Mwenyezi Mungu alivyoikamilisha umbo lake ili itekeleze kazi iliyoumbiwa nayo

8Akaibainishia njia ya shari na njia ya kheri

9Amefaulu mwenye kuisafisha na kuikuza kwa kheri

10Na ameingia kwenye hasara mwenye kuitia nafsi yake kwenye maasia

11Kabila la Thamūd lilimkanusha Nabii wake kwa kuvama kwenye uasi

12Pindi walipotoka wabaya zaidi wa kabila hilo kumchinja Ngamia. Mtume wa Mwenyezi Mungu’ Ṣāliḥ, amani imshukie

13akawaambia: «Tahadharini kumgusa kwa ubaya ngamia ambaye ni miujiza ilioletwa na Mwenyezi Mungu kwenu inayoonyesha ukweli wa Nabii wenu, na msizuie kinywaji chake. Yeye ana siku yake ya kunywa na nyinyi mna siku yenu maalumu ya kunywa.» Hilo likawa zito kwao

14Wakamkanusha na kulipuza onyo lake wakamchinja.Mola wao Akawafinika kwa adhabu, akaisawazisha juu yao na hakuna aliyeweza kuponyoka

15Wala Haogopi, Mwenye uwezo uliotukuka, athari ya adhabu kali Aliywateremshia

chanzo: Abdullah Muhammad Abu Bakr

WEBREATH · 11:11

«If you are thankful, I will give you more» — Quran 14:7

Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.

WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath