Uislamu
nyuma

90. Al-Balad

1Mwenyezi Mungu Anaapa kwa mji huu mtakatifu wa Makkah

2Na wewe, ewe Nabii, ni mkazi wa mji huu mtakatifu

3Na Anaapa kwa mzazi wa wanaadamu, ambaye ni Ādam, amani imshukie, na kilichozalikana na yeye

4Hakika Tumemuumba binadamu katika usumbufu na shida za kilimwengu

5Kwani anadhani kwa mali aliyoyakusanya kuwa Mwenyezi Mungu Hatakuwa na uwezo juu yake

6Huwa akisema kwa kujigamba: «Nimetumia mali mengi.»

7Kwani anadhani, kwa kitendo chake hiko, kuwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka na kushinda, Hamuoni wala hatamhesabu juu ya kubwa na dogo

8Kwani hatukumpa macho mawili ya kuonea

9ulimi na midomo miwili ya kusemea

10na kumfafanulia njia mbili: ya kheri na ya shari

11Basi ajiepushe na janga la Akhera kwa kutoa mali yake ili aokoke

12Ni kitu gani kilichojulisha ni lipi hilo janga la Akhera na ni mambo gani yenye kusaidia kujiepusha nalo

13Ni kuacha huru shingo iliyoamini kuikomboa na utumwa

14Au kulisha, wakati wa shida ya njaa

15yatima mwenye ujamaa, ili ipatikane fadhila ya sadaka na ya kuunga kizazi

16au masikini asiyekuwa na kitu

17Kisha akawa, baada ya kufanya amali njema zilizotajwa, ni miongoni mwa waliotakasa Imani yao kwa Mwenyezi Mungu, wakausiana kusubiri juu ya kumtii Mwenyezi Mungu kwa kufuata maamrisho Yake na kujiepusha na vitendo vya kumuasi na wakausiana kuwahurumia viumbe

18Wenye kufanya hayo ndiwo watu wa kulia ambao watapelekwa Siku ya Kiyama upande wa kulia kuelekea Peponi

19Na wale waliokanusha Qur’ani ndio ambao watapelekwa, Siku ya Kiyama, upande wa kushoto kuelekea Motoni

20Malipo yao ni Moto wa Jahanamu wenye kuwafinika na kuwaziba

chanzo: Abdullah Muhammad Abu Bakr

WEBREATH · 11:11

«If you are thankful, I will give you more» — Quran 14:7

Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.

WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath