89. Al-Fajr
1Mwenyezi Mungu Anaapa kwa wakati wa alfajiri
2na masiku kumi ya kwanza ya Mfungotatu na kwa kile kilichoyafanya yawe matukufu
3kwa kila idadi igawanyikayo na isiyogawanyika
4kwa usiku upitapo na giza lake
5Kwani hakuna katika kiapo kiliyotajwa chenye kukinaisha kwa mwenye akili
6Huoni, ewe Mtume, vipi Mola wako
7Alivyoiangamiza kaumu ya Ād'. kabila la Irama lenye nguvu na majengo yaliyoinuliwa juu ya vipia
8ambalo hakukuumbwa mfano wake katika miji, kwa ukubwa wa miili na wingi wa nguvu
9Na vipi Alivyowafanya Thamūd, kaumu ya Ṣāliḥ, ambao waliweza kuchonga jabali na kufanya nyumba ndani yake
10Na vipi Alivyomfanya Firauni, mfalme wa Misri, aliyekuwa na askari waliouhami ufalme wake na kuutilia nguvu
11Hawa ndio waliokitumia nguvu na kudhulumu mijini
12Wakaeneza humo, kwa dhuluma zao, uharibifu
13Mwenyezi Mungu Akawamiminia adhabu kali
14Hakika Mola wako,ewe Mtume, Anamwangalia mwenye kumuasi kwa kumpa muhula kidogo, kisha Humpatiliza kwa uwezo na ushindi
15Huyu binadamu, Mola wake Anapompa mtihani wa neema, Anapomkunjulia riziki yake na kumpa maisha mazuri, huwa akidhani kuwa hayo ni kwa kuwa yeye ana cheo kwa Mola wake na huwa akisema :»Mola wangu Amenitukuza.»
16Na Anapomuonja na Akambania riziki yake, huwa akidhani kuwa hayo ni kwa kuwa yeye amefanywa mnyonge na Mwenyezi Mungu na huwa akisema: «Mola wangu Amenifanya mnyonge.»
17Hali ya mambo si kama anavyodhania binadamu huyu, kwani mtu hutukuzwa kwa kumtii Mwenyzi Mungu na hufanywa mnyonge kwa kumuasi Mwenyezi Mungu. Na nyinyi hamwakirimu mayatima na kuwatendea wema
18Wala hamhimizani kulisha maskini
19Na mnakula haki za watu, katika kurithi, kwa pupa
20Na mnapenda mali kupita kiasi
21Basi hali zenu zisiwe namna hiyo. Kumbukeni pindi ardhi itakapotikiswa na kuvunjwavunjwa
22Na Akaja Mola wako kutoa uamuzi kwa waja Wake hali Malaika wamepiga safu
23Na ukaletwa, Siku Hiyo kubwa, moto wa Jahanamu. Hiyo ndiyo Siku kafiri atakumbuka na kutubia. Kutamfalia nini sasa kukumbuka kwake na kutubia, na yeye katika ulimwengu alikuwa ameyapuuza hayo, na wakati wake umekwisha kupita
24Atakuwa akisema: ‘Laiti mimi nilitanguliza ulimwenguni amali zenye kunifaa katika maisha yangu ya Akhera’
25Katika Siku Hiyo ngumu yenye vituko, hakuna atakaye kuweza kuadhibu kama adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa anayemuasi
26Na hakuna atakaye kuweza kufunga kama kifungo Chake wala kufikia hadi yake
27Ewe nafsi iliyotulia kwa kumtaja Mwenyezi Mungu, kumwamini Yeye na kuamini starehe ya Pepo Aliyowaandalia waumini
28Rudi kwa Mola wako hali ya kuridhika na takrima ya Mwenyezi Mungu kwako na hali ya kuwa Mwenyezi Mungu Ameridhika na wewe
29Ingia miongoni mwa waja wa Mwenyezi Mungu walio wema
30na ingia kwenye Pepo yangu
chanzo: Abdullah Muhammad Abu Bakr
WEBREATH · 11:11
«If you are thankful, I will give you more» — Quran 14:7
Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.
WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath