Uislamu
nyuma

88. Al-Ghaashiya

1Je, ilikujia,ewe Mtume, habari ya Kiyama chenye vituko venye kuwaenea watu

2Nyuso za Makafiri, Siku hiyo, zitakuwa zimenyongeka kwa adhabu

3Zishughulishie, zimechoka na kutaabika

4Zinachomwa kwa Moto wenye kuwaka kwa ukali

5Zitanyweshwa maji ya chemchemi yenye moto sana

6Watu wa Motoni hawatakuwa na chakula isipokuwa kinachotoka kwenye mti wa miba ilioshikana na chini. Ni kibaya sana chakula hiko na ni kichafu mno

7Hakimnoneshi mwenye kukila, awapo amekonda, wala hakimuondolei njaa, awapo na njaa

8Nyuso za Waumini, siku ya Kiyama, zitakuwa kwenye neema

9Kwa kuwa zilijishughulisha ulimwenguni kumtii Mwenyezi Mungu na kuridhika na Akhera

10Zitakuwa kwenye Pepo ya daraja ya juu

11Hutasikia humo hata neno moja la upuuzi

12Ndani yake kuna chemchemi yenye kuteremka maji yake

13Ndani yake mna vitanda vilioangatika

14na vikombe vilivyotayarishwa kwa wenye kunywa

15na mito iliyopangwa, mmoja baada ya mwingine

16na mazulia mengi yaliyotandikwa

17Kwani, hawa makafiri wenye kukanusha, hawaangalii ngamia namna walivyoumbwa kiajabu

18Na mbingu namna zlizoinuliwa juu kwa namna ya kupendeza

19Na milima namna iliyoimarishwa ukapatikana uthabiti na utulivu wa ardhi

20Na ardhi namna ilivyotandikwa na kutayarishwa

21Basi wawaidhie, ewe Mtume, wale wenye kupa nyongo yale uliyotumilizwa kwayo wala usihuzunike kwa kupa mgongo kwao

22Kwani wewe ni muwaidhiaji kwao, na si juu yako kuwalazimisha kuamini

23Lakini yule mwenye kuyapa mgongo makumbusho na mawaidha na akawa mkakamavu kwenye ukafiri wake

24Mwenyezi Mungu Atamuadhibu adhabu kali Motoni

25Hakika wao watarudi kwetu baada ya kufa

26Kisha ni juu yetu kuwalipa kwa waliyoyafanya

chanzo: Abdullah Muhammad Abu Bakr

WEBREATH · 11:11

«If you are thankful, I will give you more» — Quran 14:7

Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.

WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath