Uislamu
nyuma

87. Al-A'laa

1Takasa Jina la Mola wako Aliyetukuka na kuepukana na mshirika na kila sifa pungufu kwa namna inayonasibiana na utukufu Wake na utakatifu Wake

2Aliyeumba viumbe Akalitengeneza umbo lao na kulifanya zuri

3Na Aliyekadiria kila kitu na kukipeleka njia inayonasibiana nacho

4Na Aliyeotesha nyasi mbiti zenye rangi ya kijani

5Akazifanya baadaye kuwa kavu zilizobadilika rangi

6Tutakusomea, ewe Mtume, hii Qur’ani kisomo ambacho hutakisahau

7Isipokuwa iwapo Mwenyezi Mungu Ataka usahau kwa hekima na maslahi anayoyajua Yeye. Kwani Yeye ni Mjuzi wa yaliyo wazi na yaliyofichika, ya maneno na ya vitendo

8Tutakufanyia mapesi mambo yako yote; miongoni mwayo ni kukusahilishia kubeba majukumu ya utume na kuifanya nyepesi Dini uliyokuja nayo

9Basi wawaidhie kaumu zako, ewe Mtume, kwa namna tulivyokutayarishia ufanye kwenye wahyi ulioletewa, uwaongoze njia yenye kheri na wao na uwahusu kwa mawaidha yako wale wanaotarajiwa kuwaidhika nayo. Wala usijisumbue kuwashauri wale ambao mawidha hayawaathiri isipokuwa kuwatia ujeuri na kuwafanya wayakimbie

10Atanufaika kwa mawaidha anayemcha Mola wke

11na atajiepusha na mawaidha aliye mbaya asiyemuogopa Mola wake

12atakayeingia kwenye Moto wa Jahanamu akiadhibika kwa ukali wake

13Kisha hatakuwa ni mwenye kufa akapumzika wala ni mwenye kuishi akanufaika

14Hakika amefuzu mwenye kuisafisha nafsi yake na tabia mbovu

15na akamtaja Mwenyezi Mungu, akampwekesha, akamuomba, akafanya vitendo vya kumridhisha na akasimamisha Swala kwa nyakati zake kwa kutaka radhi za Mwenyezi Mungu na kufuata sheria Aliyoiweka

16Hakika yenu, nyinyi watu, mnafadhilisha pambo la maisha ya kilimwengu juu ya starehe za Akhera

17Na hakika ya mambo ni kuwa nyumba ya Akhera na starehe zake ni bora zaidi kuliko ulimwngu na ni yenye kusalia zaidi

18Haya mlioosimuliwa ndani ya Sura hii ni miongoni mwa yaliyotajwa kimaana katika Kurasa zilizotangulia kuteremshwa kabla ya Qur’ani

19Nazo ni Kurasa za Ibrāhīm na Mūsā, amani ziwashukie

chanzo: Abdullah Muhammad Abu Bakr

WEBREATH · 11:11

«If you are thankful, I will give you more» — Quran 14:7

Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.

WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath