86. At-Taariq
1Mwenyezi Mungu Anaapa kwa mbingu na nyota yenye kuchomoza usiku
2Na ni lipi lilokujulisha ni ukubwa gani wa nyota hiyo
3Hiyo ni nyota ing’arao na kuzagaa
4Hakuna nafsi yoyote isipokuwa amewakilishwa kwayo Malaika mwenye kuchunguza na kusjili amali zake ili ihesabiwe Siku ya Kiyama
5Basi aangalie binadamu mwenye kukanusha kufufuliwa ameumbwa kwa kitu gani? Ili ajue kuwa kurudisha umbo lake mara ya pili si vigumu kama kuumbwa mara ya kwanza
6Aliumbwa kwa manii yenye kupenyeza ndani ya uzao kwa haraka
7Yatokayo kwenye mgongo wa mwnamume na kifua cha mwanamke
8Hakika yule Aliyemuumba binadamu kwa maji haya ni muweza wa kumrudisha kwenye uhai baada ya kufa
9Siku zitakapofunuliwa wazi siri ziliofichwa na nafsi na kupambanuliwa njema na mbovu
10Binadamu hatakuwa na nguvu ya kuitetea nafsi yake wala hatakuwa na mtetezi wa kumwepushia adhabu ya Mwenyezi Mungu
11Na Anaapa kwa mbingu yenye mvua ya kukaririka
12Na ardhi yenye pasuko za kufanya mimea ichipuke
13Hakika Qur’ani ni neno lenye kupambanua baina ya haki na batili
14Na si upuuzi. Haifai kiumbe kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Akifanya hivyo atakuwa amemshirikisha Mwenyezi Mungu
15Hakika wenye kumkanusha Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na Qur’ani wanafanya vitimbi na mipango ili kuipinga haki na kuitilia nguvu batili
16Na Mimi nafanya vitimbi kuidhihirisha haki ingawa makafiri wanatukia.Usiwe na haraka nao, ewe Mtume, kutaka wateremshiwe adhabu
17Wape muhula uwangojee muda mchache wala usiwafanyie haraka, utaona adhabu itakayowafikia, mateso na maangamivu
chanzo: Abdullah Muhammad Abu Bakr
WEBREATH · 11:11
«If you are thankful, I will give you more» — Quran 14:7
Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.
WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath