Uislamu
nyuma

85. Al-Burooj

1Mwenyezi Mungu Anaapa kwa mbingu zenye njia za kupitia jua na mwezi

2Na kwa Siku ya Kiyama ambayo Amewaahidi viumbe kuwa Atawakusanya

3Na kwa shahidi, mwenye kutoa ushahidi, na mwenye kutolewa ushahidi juu yake. Mwenyezi Mungu Huapa kwa Anachokitaka. Lakini kiumbe hafai kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni ushirikina

4Wamelaaniwa waliofukua chini ya ardhi shimo kubwa ili kuwatesa Waumini

5Wakawasha moto mkubwa wenye kuni nyingi

6Wakawa wamekaa kwenye kingo za shimo hilo

7Wakishuhudia vitendo vya mateso na adhabu wanavyowafanyia Waumini

8Na hawakuwatesa mateso hayo isipokuwa wenye kuteswa walikuwa wanamuamini Mwenyezi Mungu Mshindi Asiyeshindwa, Mhimidiwa wa maneno Yake vitendo Vyake na sifa Zake

9Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi Ambaye, kutakasika na sifa za upungufu ni kwake, Anashuhudia kila kitu, hakuna kinachofichika kwake

10Hakika, wale waliowachoma kwa moto Waumini, wa kike na wa kiume, ili kuwazuia watu na dini ya Mwenyezi Mungu, kisha wasitubie, watapata, Siku ya Akhera, adhabu ya Jahanamu na watapata adhabu kali yenye kuchoma

11Wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na wakafanya amali njema, watapata Pepo ambayo chini ya majumba yake ya kifahari yapita mito. Huko ni kufaulu kukubwa

12Hakika malipizo ya Mola wako kwa maadui Zake na mateso Yake juu yao ni mazito

13Ndiye Yeye Mwenye kuanzisha kuumba na kisha kurudisha

14Ndiye Yeye Mwingi wa kusamehe kwa wenye kutubia, Mwingi wa mapenzi kwa wanaoikurubisha kwake

15Mwenye Arshi tukufu

16Mfanya Alitakalo: hakuna kitu Anachotaka kiwe kisiwe

17Je, ewe Mtume, imekufikia habari ya makundi yaliyokufuru na kukanusha Mitume walioletwa, ya

18Firauni na Thamūd, misiba na adhabu iliyowashukia? Hawakuzingatia kwa habari hiyo

19Bali waliokufuru waendelea kukanusha kwao, kama walivyokuwa waliokuja kabla yao

20Na Mwenyezi Mungu Amewazunguka kwa Ujuzi na Uweza Wake, hakuna chenye kufichika Kwake kuhusu wao na vitendo vyao. Hii Qu’ani siyo kama wanavyodai wenye kukanusha katika washirikina kuwa ni mashairi na uchawi ndipo wakaikanusha

21Bali hii ni Qur’ani kubwa iliyo tukufu

22iliyomo kwenye Ubao Uliohifadhiwa, haufikiwi na kubadilishwa wala kupotoshwa

chanzo: Abdullah Muhammad Abu Bakr

WEBREATH · 11:11

«If you are thankful, I will give you more» — Quran 14:7

Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.

WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath