Uislamu
nyuma

84. Al-Inshiqaaq

1Pindi mbingu itakapopasuka na kudhihiri mawingu katika pasuko zake Siku ya Kiyama

2Na ikatii amri ya Mola wake ya kuwa ipasuke, na inastahili kufuata amri hiyo

3Na pindi ardhi itakapotandikwa na kukunjuliwa

4Na milima yake kuvunjwa-vunjwa Siku hiyo

5Na ikatii amri ya Mola wake ya kuwa ifanye hivyo, na inastahili kufuata amri hiyo

6Ewe binadamu, wewe unaenda kwa Mwenyezi Mungu na unafanya amali nzuri na mbaya, kisha utakutana na Yeye Siku ya Kiyama. Na huna budi kupata kutoka Kwake malipo mazuri zaidi ya amali yako njema au yanayolingana na amali yako mbaya

7Yule mwenye kupewa waraka wa amali zake kwa mkono wake wa kulia

8naye ni yule aliyemuamini Mola wake, atahesabiwa hesabu pesi

9Na atarudi kwa watu wake Peponi akiwa ni mwenye furaha

10Na yule mwenye kupewa waraka wa amali zake kwa nyuma ya mgongo wake

11naye ni yule aliyemkanusha Mwenyezi Mungu, ataita maangamvu na hasara

12na ataingia Motoni

13Hakika yeye alikuwa kwa watu wake ulimwenguni ni mwenye furaha na majivuno, hafikirii mwisho wake utakuwa namna gani

14Alidhani hatarudi kwa Muumba wake, akiwa hai, kwa kuhesabiwa

15Sivyo hivyo! Mwenyezi Mungu Atamrudisha kama alivomuumba na kumlipa kwa amali zake. Kwani Yeye kwake ni Mtambuzi na kwa hali yake ni Mjuzi kuanzia Alipomuumba mpaka kumfufua

16Mwenyezi Mungu Ameapa kwa wekundu wa pambizo za mbingu wakati wa kutwa jua

17Na kwa usiku na viunbe tofauti - tofauti vya kutambaa, kuruka na kutembea kwa miguu, uliokusanya

18Na kwa mwezi ukamilikapo mwangaza wake

19Mtapitia, enyi watu, miongo mbalimbali na hali tofauti : kutoka kwenye tone la manii, kuptia pande la damu, nofu la nyama hadi kutiwa roho, mpaka kufa na mpaka kufufuliwa. Haifai kwa kiumbe kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu, afanyapo hilo atakuwa ameingia kwenye ushirikina

20Ni kitu gani kinachowazuia kumwamini baada ya aya zake kufafanuliwa kwao

21Na wana nini wao wanaposomewa Qur’ani hawamsujudii Mwenyezi Mungu wala hawajisalimishi kufuata yaliyokuja ndani yake

22Hakika tabia ya waliokufuru ni kuikanusha na kuikataa haki

23Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi zaidi wa ukaidi wao wanaouficha kwenye nyoyo zao hali wao wanajua kuwa yale yaliyoletwa na Qur’ani ni kweli

24Basi wape bishara, ewe Mtume, kuwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka na kuwa juu, Amewaandalia adhabu yenye uchungu

25Lakini wale wanaomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wakatekeleza amri waliyofaradhiwa na Mwenyezi Mungu watakuwa na malipo, Siku ya Akhera, yasiyokatika wala kupungua

chanzo: Abdullah Muhammad Abu Bakr

WEBREATH · 11:11

«If you are thankful, I will give you more» — Quran 14:7

Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.

WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath