Uislamu
nyuma

83. Al-Mutaffifin

1Adhabu kali ni ya wale wanaopunja vipimo vya vibaba na mezani

2Ambao wakinunua kwa watu cha kupimwa kwa vibaba au kwa mizani hujikamilishia wao wenyewe

3Na wakiwauzia watu kinachouzwa kwa vibaba au mizani wanapunguza vipimo

4Basi itakuwaje hali ya yule anayeiba na kupunja katika vipimo vyote hivyo, au yule anayeiba katika vipimo hivyo na huku awapunja watu vitu vyao? Hakika huyo yuwastahiki mateso zaidi kuliko wapunguzaji wa vipimo vya vibaba na mizani. Kwani hawaamini wale wapunjaji ya kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mwenye kuwafufua na kuwahesabu juu ya vitendo vyao

5katika Siku itakapokuwa na kitisho

6Siku watakaposimama watu mbele ya Mweyezi Mungu ili Awahesabu kwa machache na mengi walioyatenda, hali ya kuwa wao Siku Hiyo ni wenye kumnyenyekea Mwenyezi Mungu, Mlezi wa viumbe vyote

7Hakika marejeo ya watu waovu na makazi yao yatakuwa katika hali ya dhiki

8Na ni kipi kinachokujulidha dhiki hii ni ipi

9Hakika hiyo itakuwa ni jela ya kudumu na adhabu iliyo na uchungu. Penye jela hiyo ni pale walipoandikiwa kuwa watakwenda. Wameandikiwa na imepitishwa. Hapana kitakachozidishwa wala kupunguzwa

10Adhabu kali Siku Hiyo ni ya wale wenye kukanusha

11Wale ambao wanakanusha kuwako tukio la Siku ya Malipo

12Na wala haikanushi Siku Hiyo isipokuwa kila dhalimu mwenye madhambi mengi

13Anaposomewa aya za Qur’ani, husema, «Hizi ni hadithi za urongo za watu wa kale.» Mambo yalivyo si kama wanavyodai

14Bali hayo ni maneno ya Mwenyezi Mungu na Wahyi Wake kwa Mtume Wake

15Na hakika zimezibwa nyoyo zao zikawa hazimkubali Mwenyezi Mungu. Na kile kilichoziziba nyoyo hizo ni kufinikwa na wingi wa madhambi wanayoyafanya. Mambo hayako kama vile wanavyodai makafiri! Bali hakika wao, Siku ya Kiyama watazibwa wasimuone Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka na kushinda. Aya hii ni ushahidi kwamba Waumini watamuona Mola Wao Peponi

16Kisha hakika hao makafiri ni wenye kuingia Motoni, na wataziona na kuzihisi dharubu zake

17Kisha wataambiwa,»Haya ndiyo malipo ya yale ambayo mlikuwa mnayakanusha.»

18Ni kweli kabisa kwamba kitabu cha watu wema, nao ni wachamungu, kiko katika ngazi za juu Peponi

19Na ni kipi kinachokujulisha ni zipi hizi ngazi za juu

20Ni kitabu cha watu wema kilichopitishwa mambo yake, hakizidishwi kitu humo wala hakipunguzwi

21Wanayatazama yaliyomo ndani yake Malaika waliokurubishwa, wa kila mbingu

22Hakika wale wenye ukweli na kufuata amri za Mwenyezi Mungu watakuwa Peponi wnaneemeka

23juu ya viti vya fahari wanamwangalia Mola wao na wanaangalia yale waliyoandaliwa miongoni mwa kheri nyingi

24Unaonekana katika nyuso zao mng’aro wa neema

25Watanyweshwa tembo safi, lililotengezewa vyombo kwa ustadi na mwishowe kuna harufu ya miski

26Katika kuzipata neema hizo, nawashindane wenye kushindana

27Na kinywaji hiki, mchanganyo wake watokana na chemchemi iliyoko Peponi linalojulikana, kwa ubora wake, kwa jina la Tasnīm

28Hiyo ni chemchemi iliyoandaliwa wale waliokurubishwa kwa Mwenyezi Mungu na watajiburudisha nayo

29Hakika wale waliotenda maovu walikuwa duniani wakiwacheza shere Waumini

30Na wanapowapitia wanakonyezana kwa kuwakejeli

31Na wnaporudi, hawa waovu, kwa watu wao na jamaa zao, huwa na vihunzi na wao kwa kuwafanyia maskhara Waumini

32Na hawa makafiri wanapowaona Maswahaba wa Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, wamefuata uongofu, huwa wakisema, «Hakika hawa wamepotea kwa kumfuata Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie

33Na wala waovu hawa hawakutumwa wawe ni wachunguzi kwa Maswahaba na Mtume , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie

34Basi Siku ya Kiyama wale waliomkubali Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wakafanya vitendo vinavyolingana na sheria Zake, watawafanyia maskhara makafiri kama makafiri walivyokuwa wakiwafanyia mashara duniani

35Juu ya viti vya fahari, watakuwa Waumini wanaangalia yale Aliyowapa Mwenyezi Mungu miongoni mwa mambo matukufu na neema, wakiwa Peponi. Na neema kubwa ya zote ni kuangalia Uso wa Mwenyezi Mungu Mtukufu

36Je, wamelipwa makafiri, pindi watakapo kufanyiwa hayo, malipo muwafaka na yale waliyoyafanya duniani ya shari na madhambi

chanzo: Abdullah Muhammad Abu Bakr

WEBREATH · 11:11

«If you are thankful, I will give you more» — Quran 14:7

Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.

WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath