Uislamu
nyuma

82. Al-Infitaar

1Pindi mbingu zitakapopasuka na ukaharibika mpango wake

2Na pindi nyota zitakapoangukiana

3Na pindi Mwenyezi Mungu Atakapozifanya bahari kulipuka na maji yake kutoweka

4Na pindi makaburi yatakapogeuzwa kwa kufufuliwa waliokuwamo ndani yake

5Wakati huo itajua kila nafsi vitendo vyake vyote ilivyovifanya, vilivyotangulia na vilivyoahirika na italipwa kwa vitendo hivyo

6Ewe binadamu unayekanusha kufufuliwa! Ni kipi kilichokufanya uhadaike na ughurike kuhusu Mola wako Mpaji Mwenye kheri nyingi, Anayestahiki kushukuriwa na kutiiwa

7Kwani si Yeye Aliyekuumba, Akalisawazisha umbo lako, Akakuweka katika hali ya sawa na Akakurekibisha ili uweze kutekeleza nyadhifa zako

8katika sura yoyote ile Aliyoitaka Akakuumba

9Mambo hayako kama vile mnavyosema kwamba nyinyi mna haki ya kumuabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Bali nyinyi mnaikanusha Siku ya Hesabu na Malipo

10Na mjue kuwa wako na nyinyi Malaika wachunguzi

11watukufu kwa Mwenyezi Mungu, waandishi wa yale waliyowakilishwa kuyadhibiti. Hakiwapiti, katika vitendo vyenu na siri zenu, chochote

12Wanayajua mnayoyafanya, ya kheri au ya shari

13Hakika wachamungu wanaotekeleza haki za Mwenyezi Mungu na haki za waja wake watakuwa kwenye neema

14Hakika watu waovu waliopuuza haki za Mwenyezi Mungu na haki za waja wake watakuwa katika Moto mkali

15Ukali wake, Moto huo, utawapata Siku ya Malipo.Na wala wao hawatakuwa ni wenye kughibu

16wakawa hawamo ndani ya Moto wa Jahanamu, si kwa kutoka wala kwa kufa

17Ni kipi kinachokujuza ni upi utukufu wa Siku ya Hesabu

18Kisha ni kipi kinachokujuza ni upi utukufu wa Siku ya Hesabu

19Siku ya Hesabu, hataweza yoyote kumnufaisha yoyote. Na amri zote Siku Hiyo ni za Mwenyezi Mungu Peke yake Ambaye hakuna mwenye kumshinda, wala hakuna mwenye kumtendesha nguvu, wala hakuna mwenye kushindana na Yeye

chanzo: Abdullah Muhammad Abu Bakr

WEBREATH · 11:11

«If you are thankful, I will give you more» — Quran 14:7

Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.

WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath