Uislamu
nyuma

81. At-Takwir

1Pindi jua litakapokunjwa, na mwangaza wake ukaondoka

2Na pindi nyota zitakapopuputika na nuru yake ikafutika

3Na pindi majabali yatakapoondoshawa kwenye uso wa ardhi yakawa ni vumbi linaloenea

4Na pindi ngamia wenye mimba watakapoachwa na kupuuzwa

5Na pindi wanyama mwitu watakapokusanywa na kutangamanishwa, ili Mwenyezi Mungu Awape nafasi ya kulipizana wao kwa wao

6Na pindi bahari zitakapowashwa moto zikawa ni moto unaowaka

7Na pindi nafsi zitakapokutanishwa na mfano wake na sampuli yake

8Na pindi mtoto wa kike aliyezikwa akiwa hai atakapoulizwa, Siku ya Kiyama, suala la kumbembeleza na kumkejeli aliyemzika

9ni kwa dhambi gani ilikuwa kuzikwa kwake

10Na pindi kurasa za matendo zitakapoonyeshwa

11Na pindi mbingu zitakapong’olewa na kuondoshwa zilipokuwa

12Na pindi Moto utakapowashwa na ukawaka

13Na pindi Pepo , Nyumba ya Neema, itakaposongezewa watu wake wachamungu

14Litakapotokea hilo, itayakinisha kila nafsi na kujua kile ilichokitanguliza cha kheri au shari

15Anaapa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa nyota zinazofichika nuru yake mchana

16zinazotembea na zinazoghibu katika anga zake

17Na Anaapa kwa usiku unapojitokeza na giza lake

18Na kwa asubuhi unapojitokeza mwangaza wake

19Hakika Qur’ani ni ujumbe wa mjumbe mtukufu , naye ni Jibrili, amani imshukike

20Mwenye nguvu katika kuyapitisha yale anayoamrishwa. Mwenye cheo cha juu kwa Mwenyezi Mungu. Anayesikilizwa na Malaika

21Anayeaminiwa juu ya Wahyi anaoteremka nao

22Hakuwa Muhammad mnayemjua ni mwendawazimu

23Na kwa hakika Muhammad alimuona Jibrili anayemjia na utume katika pambizo kubwa

24Wala yeye hafanyi ubakhili katika kufikisha Wahyi

25Wala haikuwa hii Qur’ani ni neno la Shetani aliyefukuzwa na kutolewa kwenye rehema ya Mwenyezi Mungu. Lakini Qur’ani hii ni maneno ya Mwenyezi Mungu na ni Wahyi wake

26Akili zenu zawapeleka wapi katika kukanusha baada ya hoja hizi zilizo wazi na zenye nguvu

27Hayakuwa haya isipokuwa ni mawaidha kutoka kwa Mwenyezi Mungu yanapewa watu wote

28Kwa atakaye, kati yenu, kulingana juu ya haki na Imani

29Wala nyinyi hamtotaka isipokuwa kwa matakwa ya Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe wote

chanzo: Abdullah Muhammad Abu Bakr

WEBREATH · 11:11

«If you are thankful, I will give you more» — Quran 14:7

Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.

WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath