80. Abasa
1Yalidhihiri mabadiliko na mkunjiko katika uso wa Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie
2na akapa nyongo kwa sababu ya kwamba Abdallah bin Ummi Maktum alimjilia akitaka aelekezwe. Na alikuwa Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, ameshughulika kuwalingania miamba wa Kikureshi katika Uislamu
3Ni kitu gani kinakufanya wewe ujue uhakika wa jambo lake? Kwani huenda ikawa, kwa kuuliza kwake, nafsi yake itatakasika na kusafika
4Au pengine apate mazingatio zaidi na kutishika
5Basi yule alijyejitosheleza na kutouhitajia uongozi wako
6wewe ndiye unayemjali na wapulikiza maneno yake
7Na ni kitu gani kinachokupa jukumu kwako iwapo hakusafika na ukafiri wake
8Ama yule ambaye amekuwa na pupa la kukutana na wewe
9na huku anamuogopa Mwenyezi Mungu asiwe na kasoro katika kupata uongofu
10wewe unampuuza. Ilivyotakikana ufanye si kama ulivyofanya, ewe Mtume
11Hakika Sura hii ni mawaidha kwako na kwa kila anayetaka kuwaidhika
12Basi atakaye atamkumbuka Mwenyezi Mungu na kumtaja na atafuata Wahyi Wake
13Wahyi huu, nao ni Qur’ani, uko katika kurasa zilizotukuzwa
14zenye kuheshimiwa, zenye cheo cha juu
15zilizosafishwa na uchafu, uongezaji na upunguzaji
16Zilizoko mikononi mwa Malaika waandishi, mabalozi kati ya Mwenyezi Mungu na viumbe Wake, wenye maumbile mema, tabia zao ni nzuri na njema na pia matendo yao
17Amelaaniwa mtu kafiri na ataadhibiwa. Ni uovu ulioje wa ukafiri wake kwa Mola wake
18Kwani hajui ni kwa kitu gani Mwenyezi Mungu Alimuumba kwacho mwanzo wake
19Mwenyezi Mungu Alimuumba kwa maji machache, nayo ni manii. Akayakadiria miongo yake
20Kisha Akambainishia njia ya kheri na ya shari
21Kisha humkosesha uhai, na Amemuekea mahali pa kuzikiwa
22Kisha Akitaka Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na sifa mbaya, Atamhuisha na kumfufua baada ya kifo chake, kwa ajili ya kuhesabiwa na kulipwa
23Mambo siyo kama yale anayoyasema kafiri na anayoyafanya. Bado hajatakeleza Aliyomuamrisha kwayo Mwenyezi Mungu katika kuamini na kutenda wema kwa kumtii
24Na azingatie binadamu, vipi Mwenyezi Mungu Amekiumba chakula chake ambacho ndicho kinachoendeleza maisha yake
25Aone kwamba Sisi Tumeyamimina maji ya mvua juu ya ardhi kwa wingi
26Kisha Tumeipasua ardhi kwa Tulivyo vitoa kutoka humo miongoni mwa mimea tofauti
27Tukaotesha humo nafaka
28na zabibu, na nyasi za wanyama.Na mizaituni na mitende
29Na mabustani yenye miti mikubwa
30Na matunda
31na ndisha
32Mnajistareheshea kwazo, nyinyi na wanyama wenu
33Utakapokuja Ukelele wa Siku ya Kiyama, ambao utayatia uziwi, kwa kitisho chake, masikizi
34Siku mtu atakapomkimbia, kwa kitisho cha Siku Hiyo, nduguye
35na babake na mamake na
36mkewe na wanawe
37Kila mmoja Siku Hiyo, atakuwa na jambo litakalomzuia asishughulike na mwingine
38Nyuso za wenye neema, Siku Hiyo, zitakuwa ni zenye kung’ara
39zenye furaha na nderemo
40Na nyuso za watu wa Motoni zitakuwa na giza
41nyeusi, zafinikwa na unyonge
42Hao wenye kusifika na sifa hiyo ndiwo wale waliozikufuru neema za Mwenyezi Mungu na wakazikanusha aya zake na wakayakeuka Aliyoyaharamisha kwa kutenda maovu na kukiuka mipaka
chanzo: Abdullah Muhammad Abu Bakr
WEBREATH · 11:11
«If you are thankful, I will give you more» — Quran 14:7
Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.
WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath