Uislamu
nyuma

77. Al-Mursalaat

1Anaapa Mwenyezi Mungu kwa upepo unapovuma kwa mfululizo, huu baada ya huu

2Na kwa upepo wenye kuvuma kwa ukali wenye kuangamiza

3Na kwa Malaika waliopewa jukumu la mawingu, wakawa wayapeleka pale anapotaka Mwenyezi Mungu

4Na kwa Malaika wanaoshuka, kutoka kwa Mwenyezi Mungu

5na amri zinazopambanua baina ya haki na batili na halali na haramu

6Na kwa Malaika wanaoupokea wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kuuteremsha kwa Manabii Wake, unaowapa viumbe wake udhuru kutoka kwa Mwenyezi Mungu na pia onyo kutoka Kwake, ili watu wasiwe na hoja

7Hakika jambo la Kiyama mnaloahidiwa pamoja na lile la kuhesabiwa na kulipwa ni lenye kuwa hapana shaka

8Basi nyota zitakapofutwa na mwangaza wake ukaondoka

9na mbingu zitakapopasuka

10na majabali yatakapopeperuka na kukueanea huku na kule na yakawa ni mapepe yanayorushwa na upepo

11Na Mitume watapowekewa wakati na muda wa baina yao na ummah wao na kusemwe

12«Ni Siku kubwa gani Mitume wameahirishiwa?»

13Wameahirishiwa Siku ya hukumu na uamuzi baina ya viumbe

14Na nilipi lililokujulisha wewe, ewe binadamu, ni siku gani hiyo ya kutolewa uamuzi na ni zipi shida zake na vituko vyake

15Maangamivu makubwa Siku hiyo ni ya wale waliyoikanusha Siku hii iliyoahidiwa

16Kwani hatukuawaangamiza walitangulia kati ya umma waliopita kwa kuwakanusha kwao Mitume, kama vile watu wa Nūḥ, ‘Ād na Thamūd

17Kisha tutawakutanisha na wao wale waliokuja nyuma kati ya wale waliokuwa ni kama wao katika ukanushaji na uasi

18Mfano wa uangamizaji huo mkali ndivyo tutakavyowafanya wahalifu kati ya makafiri wa Makkah, kwa kumkanusha kwao Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie

19Maangamivu na adhabu kali Siku ya Kiyama kwa kila mwenye kuukanusha upweke wa Mwenyezi Mungu, unabii, kufufuliwa na kuhesabiwa

20Je kwani sisi hatukuwaumba nyinyi, enyi mkusanyiko wa makafiri, kutokana na maji dhaifu yaliyo matwevu nayo ni tone la manii

21tukayaweka maji haya kwenye mahali palipohifadhika, napo ni kizazi cha mwanamke

22mpaka kipindi maalumu kinachojulikana na Mwenyezi Mungu Aliyetukuka

23Tukaweza kumuumba, kumtia sura na kumtoa. Basi bora wa wenye kuweza ni s isi

24Maangamivu na adhabu kali Siku ya Kiyama kwa wenye kukanusha uweza wetu

25Je kwani hatukuifanya hii ardhi mnayoishi juu yake

26ikusanye juu ya mgongo wake walio hai wasiohesabika, na ndani ya matumbo yake wafu wasiodhibitika, na

27tukajaalia iwe na majabali yaliyojikita yaliyo marefu ili isitikisike na nyinyi, na tukawanywesha maji tamu yaliyo mazuri

28Maangamivu na adhabu kali Siku ya Kiyama kwa waliozikanusha neema hizi

29Wataambiwa makafiri Siku ya Kiyama, «Endeni kwenye adhabu ya moto wa Jahanamu mliokuwa mkiukanusha duniani

30Endeni mjifinike kwenye kivuli cha moshi wa moto wa Jahanamu ambacho hapo panachembuka vipande vitatu

31Kivuli hiko hakimfanyi mtu ahifadhike na joto la Siku hiyo wala hakizuii muwako wa Moto chochote

32Hakika moto wa Jahanamu unarusha macheche makubwa ya moto, kila cheche moja katika hayo ni kama jengo lililoimarishwa katika ukubwa na urefu wa kuenda juu

33Kama kwamba hizo cheche za moto wa Jahanamu zinazopaa juu ni ngamia weusi ambao rangi yao imeingia kwenye umanjano.»

34Maangamivu na adhabu kali kwa wenye kukanusha mateso yaliyoahidiwa na Mwenyezi Mungu

35Hii ndiyo Siku ya Kiyama ambayo wakanushaji hawatatamka maneno ya kuwanufaisha

36wala hawatapewa idhini ya kusema wakatoa nyudhuru, kwa kuwa hawatakuwa na udhuru wowote

37Maangamivu na adhabu kali kwa wenye kuikanusha siku hii na yaliyomo ndani yake

38Hii ni Siku ambayo Mwenyezi Mungu Atatoa uamuzi baina ya viumbe, na ukweli na ubatilifu utapambanuka. Tutawakusanya nyinyi Siku hiyo, enyi makafiri wa ummah huu, pamoja na makafiri wa mwanzo miongoni mwa ummah waliopita

39Basi mkiwa na hila za kujitoa na adhabu, tumieni hila zenu na mziokoe nafsi zenu na msukosuko wa Mwenyezi Mungu na mateso Yake

40Maangamivu na adhabu kali Siku ya Kiyama kwa wenye kuikanusha Siku ya Kiyama

41Hakika ya wale waliomuogopa Mola wao duniani na wakaiogopa adhabu Yake kwa kufuata amri Zake na kujiepusha na makatazo Yake. Wao Siku ya Kiyama watakuwa kwenye vivuli vya miti vilivyonyoka, na chemchemi za maji zinazotembea

42na matunda mengi yanayopendwa na nafsi zao ambayo wao wanastarehe nayo. Hapo waambiwe

43«Kuleni chakula chenye ladha na mnyweni kinywaji chenye kufurahisha kwa sababu ya matendo mema mliyoyatanguliza duniani.»

44Sisi, kwa mfano wa malipo hayo makubwa, tutawalipa watu wema katika matendo yao na utiifu wao kwetu

45Maangamivu na adhabu kali Siku ya Kiyama kwa wenye kuikanusha Siku ya Malipo na Hesabu, na kuzikanusha sterehe na mateso yaliyomo Siku hiyo

46Kisha Mwenyezi Mungu Akawaonya makafiri kwa kusema, «Kuleni aina ya vyakula vya ladha duniani na stareheni kwa matamanio yake yenye kumalizika kwa muda mchache, hakika nyinyi ni wahalifu kwa kumshirikisha kwenu Mwenyezi Mungu.»

47Maangamivu na adhabu kali Siku ya Kiyama kwa wenye kuikanusha Siku ya kuhesabiwa na kulipwa

48Na wanapoambiwa hawa washirikina, «Mswalieni Mwenyezi Mungu na mnyenyekeeni,» hawanyenyekei wala hawaswali, bali wanaendelea kuonyesha kiburi chao

49Maangamivu na adhabu kali Siku ya Kiyama kwa wenye kuzikanusha aya za Mwenyezi Mungu

50Iwapo wao hawataiamini hii Qur’ani, basi wataamini kitabu gani na maneno gani baada yake? Na Qur’ani yenyewe ni Kitabu kilichobainisha kila kitu, kilicho wazi katika hekima zake, hukumu zake na habari zake, chenye kushinda katika matamko yake na maana yake

chanzo: Abdullah Muhammad Abu Bakr

WEBREATH · 11:11

«If you are thankful, I will give you more» — Quran 14:7

Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.

WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath