76. Al-Insaan
1Kishampitia binadamu kipindi kirefa cha wakati kabla hajapulizwa roho ambapo hakuwa ni kita kinachotajika wala haijulikani athari yake
2Sisi tumemuumba binadamu kutokana na tone la manii la mchanganyiko wa maji ya mwanamume na maji ya mwanamke, ili tumtahini kwa lazima za kisheria baadaye, hivyo basi tumfanya ni mwenye masikio ya kusikia na macho ya kuonea, apate kuzisikia aya na kuziona dalili
3Sisi tumembainishia na kumfahamisha njia ya uongofu na upotevu na wema na ubaya ili awe ima ni mwenye kuamini na kushukuru. Au awe ni mwenye kukanusha na kukataa
4Sisi Tumewaandalia wakanushaji pingu za chuma za kuifunga miguu yao na minyororo ya kufungiwa mikono yao hadi shingo zao na moto ambao watachomwa nao
5Hakika watu wa utiifu na ukweli wa Imani wanaotekeleza haki za Mwenyezi Mungu, watakunywa, Siku ya Kiyama, kutoka kwenye kikombe ambacho ndani yake mna Pombe lililochanganywa na aina bora kabisa ya harufu nzuri, nayo ni maji ya kafuri
6Kinywaji hiki kilichochanganywa na kafuri, ni chemchemi wanayokunywa waja wa Mwenyezi Mungu, wanaitumia na kuipitisha wanavyotaka mapitisho mazuri
7Hao walikuwa huko duniani wanatekeleza kile walichojilazimisha nafsi zao cha utiifu kwa Mwenyezi Mungu, na wakiogopa mateso ya Mwenyezi Mungu, Siku ya Kiyama, ambayo madhara yake ni hatari na ubaya ni wenye kusambaa na kuenea kwa watu isipokuwa wale ambao Mwenyezi Mungu Amewarehemu
8Na wanalisha chakula, pamoja na kuwa wanakipenda na kukihitajia, kumpa fukara asiyeweza kuchuma, asiyemiliki chochote katika vitu vya kilimwengu, na kumpa mtoto aliyefiliwa na babake kabla ya kubaleghe na asiye na mali, na kumpa mtu aliyetekwa vitani miongoni mwa washirikina na wengineo
9na huku wanasema katika nafsi zao, «Hakika sisi tunawafanyia wema kwa kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu na kutaka malipo yake. Hatutaki badala wala hatukusudii kushukuriwa wala kusifiwa na nyinyi
10Kwa kweli, sisi tunaiogopa, kutoka kwa Mola wetu, Siku ngumu ambayo ndani yake nyuso zitakunjana na mapaji yatasinyaa kutokana na mambo yake mazito na vituko vyake vikubwa
11Basi hao Mwenyezi Mungu Atawaokoa na shida za Siku hiyo na Atawapa uzuri na mwangaza katika nyuso zao na furaha ndani ya nyoyo zao
12na Atawalipa, kwa kuvumilia kwao duniani juu ya utiifu, Pepo iliyo kubwa ambayo kutoka humo watakula wanachokitaka na watavaa humo hariri nyororo
13hali ya kuwa wametegemea juu ya vitanda vilivyopambwa kwa nguo na pazia za fahari. Hawataona humo joto la jua wala ukali wa baridi
14Na karibu nao, kutakuwa na miti ya Pepo yenye kuwafinika ambayo wamerahisishiwa kuyachuma matunda yake
15Watawazunguka wao watumishi wakiwa na vyombo vya vyakula vya fedha, na vikombe vya vinywaji vya ukoa
16ukowa wa fedha, ambavyo wanyweshaji wamevima kadiri ya watakavyotamani wenye kunywa, haviongezeki wala havipungui
17Na watu wema hawa watanyweshwa Peponi kikombe kilichijazwa Pombe iliyochanganywa na tangawizi
18watakunwa kutoka kwenye chemchemi iliyoko Peponi inayoitwa Salsabīl, kwa kuwa kinywaji chake kina usalama na kuwa kina ulaini na ladha ya kupendeza
19Na watawazunguka wema hawa wakiwatumikia wavulana wenye hali moja ya kudumu, ukiwaona utawadhania, kwa uzuri wao na usafi wa rangi zao na mng’aro wa nyuso zao, kuwa ni lulu iliyotenganishwa inayong’ara
20Na utazamapo mahali popote katika Pepo utaona starehe isiyosifika na ufalme mkubwa uliop mkunjufu usiosiokuwa na mwisho
21Juu ya miili yao pana nguo zilizoipamba, ambazo sehemu zake za ndani kuna hariri nyembamba ya rangi ya kijani, na nje yake kuna hariri nene. Na miongoni mwa mapambo watakayovishwa ni makuku ya fedha. Na Mola wao Atawanywesha, juu ya sterehe hizo, kinywaji kisicho na uchafu wala rojo
22Na wataambiwa, «Hakika nyinyi mmetayarishiwa haya yakiwa ni badala ya matendo yenu mema, na matendo yenu duniani yalikuwa ni yenye kukubaliwa na kuridhiwa na Mwenyezi Mungu.»
23Hakika sisi tumekuteremshia Qur’ani, ewe Mtume, materemsho yanayotoka kwetu, ili uwakumbushe watu yale yaliyomo ndani ya maagizo mema, matahadharisho ya ubaya, malipo mazuri na mateso
24Basi yavumilie maamuzi ya Mola Wako Aliyokupangia na uyakubali, na usonge mbele kufuata maamrisho yake ya Kidini, na usiwatii washirikina waliovama kwenye matamanio au waliokolea kwenye ukafiri na upotevu
25na uendelee kutaja jina la Mola wako na kumuomba mwanzo wa mchana na mwisho wake
26Na wakati wa usiku, mnyenyekee Mola wako na umswalie na umuabudu kipindi kirefu cha usiku
27Kwa hakika hawa washirikina wanaupenda ulimwengu na wanaushughulikia, na wanakuacha nyuma ya migongo yao kule kufanya matendo ya kuwafaa Akhera na kuwaokoa katika Siku yenye shida kubwa
28Sisi Ndio tuliowaumba na tukalipa uthabiti umbo lao. Na tunapotaka tunawaangamiza na kuwaleta watu walio watiifu zaidi wa Mwenyezi Mungu kuliko wao
29Hakika ndani ya sura hii, kwa yaliyomo ya kuvutia na kuogopesha, ya kuahidi mema na kuonya mabaya, kuna mawaidha kwa viumbe wote. Basi mwenye kujitakia wema nafsi yake ya duniani na Akhera, na ashike njia ya Imani na uchamungu itakayomfikisha kwenye msamaha wa Mwenyezi Mungu na radhi Zake
30Na hamtataka jambo lolote miongoni mwa mambo isipokuwa kwa makadirio ya Mwenyezi Mungu na matakwa Yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa hali za viumbe Vyake, ni Mwingi wa hekima katika uendeshaji na utengezaji Wake
31Anamuingiza Anayemtaka miongoni mwa waja Wake katika rehema Yake na radhi Yake, na wao ni wale walioamini. Na Amewaandalia madhalimu waliokiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu adhabu yenye kuumiza
chanzo: Abdullah Muhammad Abu Bakr
WEBREATH · 11:11
«If you are thankful, I will give you more» — Quran 14:7
Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.
WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath