Uislamu
nyuma

75. Al-Qiyaama

1Anaapa Mwenyezi Mungu kwa Siku ya Hesabu na Malipo

2na Anaapa kwa nafsi yenye kuamini na kuchamungu, inayomlaumu mwenyewe kwa kuacha matendo ya utiifu na kufanya matendo yenye kuangamiza, kwamba watu watafufuliwa

3Je anadhanihuyu binadamu kafiri kuwa sisi hatutaweza kuikusanya mifupa yake baada ya kuwa mbalimbali

4Ndio! Tutaikusanya na tunaweza kufanya vidole vyake au ncha za vidole vyake- baada ya kuvikusanya na kuzioanisha- viwe kwenye umbo la sawasawa, kama vilivyokuwa kabla ya kufa

5Bali binadamu anakanusha kufufuliwa, anataka asalie kwenye kufanya ubaya kwa siku za mbeleni za maisha yake

6Kafiri huyu huwa akiuliza, akiliona jambo la kusimama Kiyama kuwa liko mbali, «Ni lini Siku ya Kiyama?’

7Basi macho yatakapoduwaa na yakashituka kwa kutishika na kile yalichokiona cha vituko vya Siku ya Kiyama

8na ukafutika mwangaza wa mwezi

9na vikakusanywa jua na mwezi katika kukosa mwangaza, kikawa kila mojawapo ya hivyo viwili hakina mwangaza

10wakati huo binadamu atasema, «Pa kukimbilia ni wapi kuiepuka adhabu?»

11Mambo sivyo kama unavyotamani yawe, ewe binadamu, ya kutaka kukimbia. Huna mahali pa kukimbilia wala pa kupata uokozinfsi yake

12Kwa Mwenyezi Mungu Peke Yake ndio mwisho wa viumbe Siku ya Kiyama na ndipo mahali pao pa kutulia, na hapo Amlipe kila mtu kwa kile alichostahiki

13Atapashwa habari binadamu Siku hiyo kwa matendo yake yote, mema na mabaya, aliyoyatanguliza miongoni mwa hayo katika maisha yake na aliyoyachelewesha

14Bali binadamu ni hoja iliyo wazi juu ya nafsi yake, yenye kumfuata kwa alichokitenda na alichokiacha

15hata kama atakuja na kila udhuru wa kuelezea sababu ya uhalifu wake, hilo halitamfaa

16Usitikise, ewe Nabii, ulimi wako kwa Qur’ani wakati wahyi unapoteremka ili ufanye haraka kuihifadhi kwa kuogopa isikuponyoke

17Kwani ni juu yetu sisi kuikusanya kwenye kifua chako kisha uisome kwa ulimi wako wakati utakapo. Mjumbe wetu Jibrili akikusomea

18basi kisikilize kisomo chake na umpulikize. Kisha isome kama alivyokusomea

19kisha ni juu yetu kukuelezea kilichokutatiza kukifahamu katika maana yake na hukumu zake

20Mambo sivyo kama mlivyodai, enyi mkusanyiko wa washirikina, kuwa hakuna kufufuliwa wala kulipwa

21Bali nyinyi ni watu mnaopenda dunia na pambo lake na mnaacha Akhera na starehe zake

22Nyuso za watu wema Siku ya Kiyama zitakuwa ni zenye kung’ara, nzuri na zenye furaha

23zitamuona Mola Aliyeziumba na Anayezimiliki, na zitastarehe kwa hilo

24Nyuso za watu wabaya Silku ya Kiyama zitakuwa ni zenye kukunjana na kusinyaa

25zinatazamia kushukiwa na msiba mkubwa wenye kuvunja

26Ni kweli! Pindi roho itakapofika sehemu za juu za kifua

27na wakasema baadhi ya waliohudhuria kuwaambia wengine, «Je kuna mtu wa kumzungua na kumpoza kutokana na hali hii aliyonayo?»

28Na yule ambaye yuko katika hali ya kufa akajua kwamba lile lililomshukia ni kuaga dunia, kwa kuwa anawaona Malaika wa mauti

29Na ikashikana shida ya mwisho wa duniani na shida ya mwanzo wa Akhera. Kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka

30Watu watapelekwa Siku ya Kiyama: ima Peponi au Motoni

31Hakuwa kafiri ni mwenye kumuamini Mtume na Qur’ani, wala hakuwa ni mwenye kumtekelezea Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Swala za faradhi

32Lakini aliikanusha Qur’ani na akaipa mgongo Imani

33kisha akaenda kwa watu wake akijiona hali ya kujigamba katika kutembea kwake. Basi maangamivu

34ni yako baada ya maangamivu

35Kisha maangamivu ni yako baada ya maangamivu

36Je anadhani huyu binadamu anayekanusha kufufuliwa kuwa ataachwa bure: haamrishwi wala hakatazwi, hahesabiwi wala hateswi

37Kwani hakuwa binadamu huyu ni tone la manii dhaifu linalotokana na maji matwevu yanayomwagwa na kumiminwa kwenye kizazi

38kisha yakawa ni kipande cha damu iliyo kavu. Mwenyezi Mungu Akaliumba kwa uweza Wake na Akazilinganisha sura zake katika umbo la mwili lililo zuri kabisa

39Akafanya kutokana na binadamu huyu jinsi mbili: ya kiume na ya kike. Je kwani hakuwa Mola huyo Muumba wa vitu hivyo ni Muweza wa kuwarudisha viumbe wakiwa hai baada ya kutoweka kwao

40Ndio! Anaweza. Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, kwa hakika ni Muweza wa hilo

chanzo: Abdullah Muhammad Abu Bakr

WEBREATH · 11:11

«If you are thankful, I will give you more» — Quran 14:7

Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.

WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath