Uislamu
nyuma

69. Al-Haaqqa

1Kiyama chenye kutukia kikweli ambacho ndani yake inahakikika ahadi ya Mwenyezi Mungu na onyo Lake

2Kiyama chenye kutukia kikweli ni zipi sifa zake na hali zake

3Na kitu gani kilichokujulisha wewe, ewe Mtume, na kukueleza uhakika wa Kiyama na kikakupa wewe picha ya janga lake na shida zake

4Thamūd, nao ni watu wa Ṣāliḥ, na ‘Ād, nao ni watu wa Hūd, walikikanusha Kiyama ambacho kinagonga nyoyo kwa vituko janga lake

5Ama hao Thamūd waliangamizwa kwa ukelele mkubwa uliopita kiasi ukali wake

6na ama‘Ād waliangamizwa kwa upepo baridi unaovuma kwa nguvu

7Mwenyezi Mungu Aliwasaliti nao masiku saba na michana minane yenye kufuatana, isiyokatika wala kusimama. Utawaona watu katika masiku hayo na michana wamekufa, kama kwamba wao ni vigogo mitende iliyo mibovu iliyolika ndani

8Basi je utamuona mtu yoyote miongoni mwao mwenye kusalia bila kuangamia

9Na akaja mpita kiasi katika uasi Fir’awn na ummah waliomtangulia waliokanusha Mitume wao, na watu wakazi wa vijiji vya watu wa Lūṭ ambao majumba yao yaliwapindukia kwa sababu ya kitendo kibaya walichokifanya, cha ukafiri, ushirikina na mambo machafu

10Kila ummah kati yao walimuasi mjumbe wa Mola wao ambaye alitumwa kwao, basi Mwenyezi Mungu Akawashika mshiko mkali mno

11Sisi, maji yalipopita kipimo chake, mpaka yakawa juu na kuangatika juu ya kila kitu, tuliwabeba watu wa asili zenu pamoja na Nūḥ ndani ya jahazi ambayo ilikuwa ndio sababu ya kuokoka Waumini na kuzamishwa makafiri

12hili likiwa ni mazingatio na mawaidha, na lipate kulihifadhi tukio hilo kila shikio ambalo kazi yake ni kuhifadhi, na lielewe kile ambacho limekisikia

13Pindi Malaika atakapopuliza kwenye barugumu mpulizo mmoja, nao ni mpulizo wa kwanza ambao hapo patapatikana maangamivu ya ulimwengu

14Na pindi ardhi na milima itakapoinuliwa kutoka mahali ilipo ikavunjwavunjwa na kugongwagongwa mara moja

15Wakati huo Kiyama kitasimama

16Na mbingu zitafanya ufa na ziwe dhaifu na kulegea Siku hiyo, hazitakuwa na mshikamano wala ugumu

17Na Malaika watakuwa kwenye pambizo na pande zake, na wataibeba «Arshi ya Mola wako juu yao Siku ya Kiyama Malaika wanane miongoni mwa Malaika wakubwa

18Katika Siku hiyo, mtaorodheshwa kwa Mwenyezi Mungu, enyi wat, ili mhesabiwe na mlipwe, hakuna chochote kitakachofichamana kwa Mwenyewzi Mungu miongoni mwa siri zenu

19Ama yule Atakayepewa kitabu cha matendo yake kwa mkono wake wa kulia, atasema akiwa katika hali ya ubashasha na furaha, ‘Chukueni kitabu changu mkisome

20Mimi nilikuwa na yakini duniani kuwa nitapata malipo yangu Siku ya Kiyama, nikajiandalia nayo kwa matayarisho ya Imani na matendo mema.»

21Basi yeye atakuwa kwenye maisha ya furaha ya kumridhisha

22kwenye Pepo ya juu kimahali na daraja

23matunda yake yako karibu, anayachuma anayesimama, anayeketi na anayelala

24Wataambiwa, «Kuleni na mnyweni kila aina ya vyakula na vinywaji, mkiwa mbali na kila kero, mkiwa mmesalimika na kila mnalolichukia, kwa sababu ya matendo mema mliyoyatanguliza siku za ulimwenguni.»

25Na ama yule atakayepewa kitabu cha matendo yake kwa mkono wake wa kushoto

26atasema akiwa katika hali ya kujuta na kupata hasara

27«Natamani lau mimi sikupewa kitabu changu na sikujua malipo yangu! Natamani lau kile kifo nilichokufa duniani kilikuwa ndicho chenye kukata kabisa mambo yangu na nisifufuliwe baada yake

28Mali yangu niliyoyakusanya hayakuninufaisha duniani

29Hoja zangu zote zimenionokea, na sina hoja tena ya kuitumia kama hoja.»

30Hapo waambiwe walinzi wa Moto wa Jahanamu, «Mchukueni mhalifu huyu mfanya dhambi, ikusanyeni mikono yake shingoni mwake muitie pingu

31kisha mtieni kwenye Moto unaowaka sana, apate kulihisi joto lake

32Kisha mfungeni mnyororo wa chuma ambao urefu wake ni dhiraa sabini mumkokote nao na mumtie humo

33Kwani yeye hakuwa akiamini kuwa Mwenyezi Mungu Ndiye Mola wa Haki, Peke Yake, Asiye na mshirika

34Wala hakuwa akitenda matendo yanayoambatana na uongofu Wake, wala hakuwa akiwahimiza watu duniani kuwalisha wenye uhitaji miongoni mwa masikini na wengineo

35basi kafiri huyu Siku ya Kiyama hatakuwa na jamaa wa karibu wa kumuepushia adhabu

36wala hatakuwa na chakula isipokuwa kile kinachotokana na usaa wa watu wa motoni

37hakuna mwenye kukila isipokuwa wale wenye dhambi, wanaoshikilia kumkanusha Mwenyezi mungu

38Naapa kwa mnavyoviona miongoni mwa vitu vinavyooonekana

39na vile msivyoviona miongoni mwa vile vilivyoghibu kwenu., hakika Qur’ani ni maneno ya Mwenyezi Mungu

40Inasomwa na mjumbe mkubwa wa cheo na utukufu

41Na si maneno ya mshairi kama mnavyodai, ni uchache mno mnavyoamini

42Wala si tungo kama zile tungo za makuhani, ni kuchache mno kule kukumbuka kwenu na kutia akilini kuwa kuna tafauti baina ya mawili hayo

43Lakini hiyo Qur’ani ni maneno ya Mola wa viumbe wote Aliyoyateremshia Mtume Wake Muhaammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie

44Na lau Muhammad angalitusingizia maneno tusiyoyanena

45tungalimtesa na tungalimkamata kwa nguvu na uweza, kwani nguvu ya kila kitu iko kwenye upande wake wa kulia

46kisha tungalimkata mshipa wa moyo wake

47hataweza yoyote kuyazuia mateso yetu yasimpate

48Na hii Qur’ani ni mawaidha kwa wachamungu wanaofuata amri za Mwenyezi Mungu na kuyaepuka makatazo yake

49Na sisi kwa hakika tunajua kwamba miongoni mwenu kuna wanaoikanusha hii Qur’ani pamoja na kuwa dalili zake ziko wazi

50Na kwa hakika kuikanusha Qur’ani ni majuto makubwa kwa wenye kuikanusha pindi watakapoiona adhabu yao na kuona starehe za wenye kuiamini

51Na kwa hakika hii Qur’ani ni haki iliyothibiti na yakini isiyo na shaka

52Basi Mwepushie Mwenyezi Mungu, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, kila sifa isiyonasibiana na haiba Yake, na umtaje kwa jina Lake tukufu

chanzo: Abdullah Muhammad Abu Bakr

WEBREATH · 11:11

«If you are thankful, I will give you more» — Quran 14:7

Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.

WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath