55. Ar-Rahmaan
1mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema
2Amemfundisha binadamu Qur’ani kwa kurahisisha kuisoma, kuihifadhi na kuelewa maana yake
3Amemuumba binadamu
4Amemfundisha ufasaha wa kujieleza ili kumtenganisha na wengine
5Jua na mwezi zinatembea kwa kufuatana, moja baada ya nyingine, kwa hesabu madhubuti isiyotafautiana wala kugongana
6Na nyota iliyo mbinguni na miti ya ardhini, vinamjua Mola wao, vinamsujudia na vinanyosha shingo zao kufuata vile ambavyo vimepangiwa vifuate vya maslahi ya waja Wake na manufaa yao
7Na mbingu Ameiinua na kuifanya iwe juu ya ardhi, Na Ameweka kwenye ardhi uadilifu Aliouamrisha na kuulazimisha kwa waja Wake
8Ili msipite mipaka na msimfanyie hiyana mnayempimia
9Na simamisheni upimaji kwa usawa na msipunguze mizani mnapowapimia watu
10Na ardhi Ameiweka na Ameitayarisha, ili viumbe vitulie juu yake
11Humo mna matunda na mitende yenye makarara ya matunda. Na humo kuna nafaka zenye maganda, vikiwa ni chakula chenu na wanyama wenu
12Na humo mna kila mmea wenye harufu nzuri
13Bas ni neema gani za Mola wenu, za kidini na za kidunia, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha? Na ni jawabu nzuri ilioje ya majini alipowasomea wao Nabii, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, sura hii, kila akipita kwenye aya hii walikuwa wakisema, «Hakuna chochote miongoni mwa neema zako, ewe Mola wetu, tunachokanusha. Sifa njema zote ni zako.» Na hivi ndivyo inavyotakiwa kwa mja anapoelezewa neema za Mwenyezi Mungu na mema Yake akubali na amshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema hizo
14Amemuumba baba wa wanadamu, naye ni Ādam, kwa udongo mkavu kama vyungu
15Na Amemuumba Iblisi, naye ni katika majini, kwa mroromo wa moto uliochanganyika
16Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha
17Mola wa pande mbili za Mashariki ya jua, katika kusi na kaskazi, na Mola wa pande mbili za Magharibi ya jua, katika kusi na kaskazi, kwani vyote viko chini ya uendeshaji Wake na ulezi Wake
18Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha
19Mwenyezi Mungu Ameyachanganya maji ya bahari mbili, tamu na chumvi, yanakutana, baina yake kuna kizuizi
20mojawapo haiingii sehemu ya nyingine na kuiondoa sifa yake, bali ya tamu inasalia kuwa tamu na ya chumvi inasalia kuwa chumvi pamoja na kukutana kwake
21Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha
22Inatoka kwenye bahari mbili hizo, kwa uweza wa Mwenyezi Mungu, lulu na marjani
23Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha
24Ni Yake Yeye, Aliyetakasika na kutukuka, mamlaka ya kuyaendesha majahazi makubwa yanayotembea baharini kwa manufaa ya watu, yenye kusimamisha juu milongoti yake na matanga yake kama vile majabali
25Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu mnazikanusha
26Kila aliye juu ya uso wa ardhi miongoni mwa viumbe ni mwenye kuangamia
27na utasalia uso wa Mola wako Mwenye utukufu, ubora, kheri nyingi na upaji. Katika aya hii pana kuthibitisha sifa ya uso kwa Mwenyezi Mungu kwa namna inavyonasibiana na Yeye, kutakasika ni Kwake, bila kufananisha wala kueleza namna ulivyo
28Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha
29Wanamuomba Yeye walioko mbinguni na ardhini haja zao. Hakuna yoyote anayejitosheleza kutomhitajia Yeye, kutakasika ni Kwake. Kila siku Yeye Yuko kwenye jambo: Anatukuza na Anatweza, Anatoa na Anazuia
30Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha
31Nitawatengea kipindi cha kuwahesabu na kuwalipa kwa matendo yenu mliyoyafanya, enyi vizito viwili:-majini na binadamu-, tuwatese watu wa maasia na tuwape malipo mema watu wa utiifu
32Ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha
33Enyi mkusanyiko wa majini na binadamu! Mkiweza kuihepa amri ya Mwenyezi Mungu na uamuzi Wake kwa kukimbia kwenye pambe za mbingu na ardhi basi fanyeni, na hamuwezi kufanya hivyo isipokuwa kwa nguvu na hoja na amri inayotoka kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka. (Na vipi mtaweza kufanya hivyo na hali nyinyi hamzimilikii nafsi zenu manufaa yoyote wala madhara)
34Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha
35Mtatumiwa mroromo wa moto na shaba iliyoyayushwa, mmiminiwe juu ya vichwa vyenu msiweze kusaidiana
36Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazukanusha
37Na pindi mbingu itakapopasuka na kuachana Siku ya Kiyama, ikawa nyekundu kama rangi ya waridi na kama mafuta yaliyochemshwa na risasi iliyoyayushwa, kutokana na mambo magumu na vituko vya Siku ya Kiyama
38Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha
39Katika Siku hiyo Malaika hawatawauliza wale wahalifu, miongoni mwa binadamu na majini, kuhusu dhambi zao
40Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha
41Malaika watawajua wahalifu kwa alama zao, hapo wawashike kwenye paa za vichwa vyao na nyayo zao wawarushe Motoni
42Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha
43Wataambiwa hao wahalifu kwa njia ya kulaumiwa na kudhalilishwa, «Huu ndio moto wa Jahanamu ambao wahalifu duniani walikuwa wakiukanusha
44mara wanaadhibiwa kwenye Jaḥīm, na mara nyingine wananyweshwa Hāmīm, nacho ni kinywaji kilichofikia upeo wa ukali wa moto, kinakata tumbo na sehemu za ndani ya mbavu
45Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu mnazikanusha
46Na anayemcha Mwenyezi Mungu, miongoni mwa waja Wake binadamu na majini, akaogopa kusimama kwake mbele Yake, akamtii na akaacha kumuasi atakuwa na mabustani mawili ya Pepo
47Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha
48Mabustani mawili hayo ya Pepo yana matawi yaliyostawi kwa matunda ya kila aina
49Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha
50Katika Pepo mbili hizo kuna chemchemi mbili za maji zinazopita katikati yake
51Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha
52Katika mabustani hayo mawili ya Pepo kuna sampuli mbili za kila aina ya matunda
53Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha
54Na wale wanaoogopa kusimama mbele ya Mola Wao watakuwa na mabustani mawili ya Pepo, ambayo ndani yake watastarehe, hali ya kutegemea juu ya matandiko yaliyojazwa dibaji nzito. Na matunda ya mabustani mawili hayo ya pepo yako karibu nao
55Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mtazikanusha
56Katika matandiko hayo wapo wake macho yao yanawatazama waume zao tu, hawawatazami wengineo, wamefungamana na wao. Hakuna aliyewaingilia, kabla ya hao waume zao, binadamu yoyote wala jini
57Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadanu, mnazikanusha
58Kama kwamba hawa wake wa kihurulaini ni yakuti na marijani katika sifa zao na uzuri wao
59Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa najini na binadamu , mnazikanusha
60Je atakuwa na malipo yoyote, huyu aliyekuwa mwema wa matendo duniani, isipokuwa ni afanyiwe wema kwa kupewa Pepo huko Akhera
61Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha
62Na chini ya mabustani ya Pepo mawili yaliyotangulia kuna mabustani ya Pepo mawili mengine
63Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha
64Mabustani haya mawili ni rangi ya kijani. Ujani wake umeiva sana mapaka umeingia kwenye weusi
65Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha
66Ndani ya mabustani mawili hayo ya Peponi kuna chemchemi mbili zenye kububujika maji daima bila kukatika
67Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha
68Kwenye mabustani hayo mawili kuna aina za matunda, mitende na mikomamanga
69Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha
70Ndani ya mabustani haya manne ya Pepo kuna wake walio wema wa tabia na wazuri wa nyuso
71Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha
72Mahurulaini wakunjufu wa macho, waliositiriwa na kuhifadhiwa mahemani
73Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha
74Hawajaingiliwa Mahurulaini hawa na binadamu yoyote wala jini kabla ya waume zao
75Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha
76Hali ya kuwa wametegemea kwenye mito yenye mifuko rangi ya kijani na matandiko mazuri
77Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha
78Zimekithiri mno baraka za Jina la Mola wako, na kheri Zake zimekuwa nyingi, Mwenye haiba kubwa, utukufu wenye kukamilika na takrima kwa wenye kumtegemea Yeye
chanzo: Abdullah Muhammad Abu Bakr
WEBREATH · 11:11
«If you are thankful, I will give you more» — Quran 14:7
Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.
WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath