Uislamu
nyuma

111. Al-Masad

1Imehasirika mikono miwili ya Abu Lahab, na yeye mwenyewe ameangamia, kwa kumuudhi Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie. Hasara ya Abu Lahab ilithubutu

2Hayakumfalia kitu mali yake na watoto wake. Kwani hivyo havitamkinga na adhabu ya Mwenyezi Mungu pindi ikimshukia

3Ataingia kwenye Moto wenye kuroroma

4yeye na mke wake ambaye alikuwa akibeba miba na kuiweka kwenye njia anayopita Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, ili kumuudhi

5Kwenye shingo yake patakuwa na kamba imara ya lifu gumu lilio kavu; atabebewa nayo kwenye Moto wa Jahanamu, kisha atarushwa nayo mpaka chini

chanzo: Abdullah Muhammad Abu Bakr

WEBREATH · 11:11

«If you are thankful, I will give you more» — Quran 14:7

Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.

WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath