107. Al-Maa'un
1Je, waiona hali ya yule ambaye akanusha kufufuliwa na kulipwa
2Huyo ndiye yule anayemkaripia yatima kwa nguvu akimnyima haki yake kwa sababu ya ususuavu wa moyo wake
3Na wala hawahimizi wengine kulisha masikini. Vipi yeye mwenyewe atamlisha
4Basi adhabu kali itawafikia wenye kusali
5ambao wameghafilika na Swala zao: hawazisimamishi kama ipasavyo wala hawazisali kwa nyakati zake
6Ambao huonyesha watu amali zao za kheri kwa njia ya ria
7Na wanakataa kuwaazima watu vitu ambavyo hawadhuriki kwa kuviazima, kama vyombo vya kutumia na vinginevyo. Wao hawakujifanyia wema nafsi zao kumuabudu Mola wao wala hawakuwafanyia wema viumbe Vyake
chanzo: Abdullah Muhammad Abu Bakr
WEBREATH · 11:11
«If you are thankful, I will give you more» — Quran 14:7
Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.
WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath