106. Waquraishi
1Oneni ajabu ya mazowea ya Makureshi, amani walionayo, kuwaendea uzuri mambo yao
2kupangika na kusahilika misafara yao ya kwenda Yamani kipindi cha kusi na kwenda Shamu kipindi cha kaskazi, ili kuleta vitu wanavyohitajia
3Basi, wamshukuru na kumuabudu Bwana wa Nyumba hii ya Alkaba, Ambaye kwa ajili Yake wametukuzwa, na wampwekeshe na kumtakasia ibada
4Ambaye Amewapa wao chakula wakati wa njaa kali na akawapa amani na utulivu kutokana na kicho kikubwa na babaiko
chanzo: Abdullah Muhammad Abu Bakr
WEBREATH · 11:11
«If you are thankful, I will give you more» — Quran 14:7
Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.
WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath