Uislamu
nyuma

104. Al-Humaza

1Shari na maangamivu yatampata kila mwenye kusengenya watu na kuwatukana

2Ambaye hamu yake ni kukusanya mali na kuyahesabu

3Akidhani kuwa mali yake ambayo ameyakusanya yatampa dhamana ya kuishi milele duniani na kuhepa kuhesabiwa

4Anavyodhania sivyo. Atatiwa ndani ya Moto ambao huvunjavunja kila kinachotiwa

5Lipi lililokujulisha, ewe Mtume, ni upi huo Moto unaovunjavunja

6Huo ni Moto wa Mwenyezi Mungu uliowashwa

7Ambao kwa ukali wake hupenyeza miilini ukafikia kwenye nyoyo

8Moto huo umefungiwa juu yao wakiwa wametiwa minyororo

9na pingu ndefu ili wasitoke

chanzo: Abdullah Muhammad Abu Bakr

WEBREATH · 11:11

«If you are thankful, I will give you more» — Quran 14:7

Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.

WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath