102. At-Takaathur
1Kumewashughulisha kujifahiri kwa mali na watoto mkawacha kumtii Mwenyezi Mungu
2Kujishughulisha kwenu na hilo kumeendelea mpaka mkawa makaburini na mkazikwa humo
3Siyo namna hii inatakiwa iwapumbaze kushindana kwa wingi wa mali. Itawadhihirikia kuwa Nyumba ya Akhera ni bora kwenu
4Kisha tahadharini mtajua mwisho mbaya wa kutojishughulisha na Akhera
5Siyo namna hii inatakiwa iwashughulishe kushindana kwa wingi wa mali.Lau mnajua kikweli, mngalirudi nyuma na mngaliangusiliza kuokoa nafsi zenu kutoka kwenye maangamivu
6Mtauona Moto
7Kisha mtauona bila shaka
8Kisha mtaulizwa kuhusu kila aina ya starehe mliyokuwa nayo
chanzo: Abdullah Muhammad Abu Bakr
WEBREATH · 11:11
«If you are thankful, I will give you more» — Quran 14:7
Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.
WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath