101. Al-Qaari'a
1Kiyama chenye kugonga nyoyo za watu kwa vituko vyake
2Ni kitu gani hiko chenye kugonga
3Na ni lipi lililokujulisha ni kipi hiko chenye kugonga
4Siku hiyo watu watakuwa , kwa wingi wao, kugawanyika kwao na kuzunguka kwao, ni kama pandzi walioenea. Nao ni wale wanaojitupa motoni
5Na majabali yatakuwa ni kama pamba yenye rangi tofauti inayochambuliwa kwa mkono ikawa ni mapepe na ikamalizika
6Basi mwenye kuwa mizani za mema yake ni nzito
7atakuwa kwenye maisha ya kuridhika Peponi
8Ama mwenye kuwa mizani za mema yake ni nyepesi na mizani za maovu yake ni nzito
9makazi yake yatakuwa ni Moto wa Jahanamu
10Ni lipi lililokujulisha, ewe Mtume, ni ipi hii Jahanamu inayoitwa «Hāwiyah»
11Ni Moto unaowaka sana kwa kuni ziliomo ndani yake
chanzo: Abdullah Muhammad Abu Bakr
WEBREATH · 11:11
«If you are thankful, I will give you more» — Quran 14:7
Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.
WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath