100. Al-Aadiyaat
1Mwenyezi Mungu Anaapa kwa farasi wenye kwenda shoti katika njia Yake kumkabili adui, wakitoa sauti kwa kasi ya kukimbia. Haifai kwa kiumbe kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni ushirikina
2Na wenye kutoa cheche za moto kwa kwato zao ngumu wanapokimbia kwa kasi
3Wenye kushambulia maadui kipindi cha asubuhi
4Wakarusha vumbi kwa mbio zao
5Wakautia kati, kwa kuuzunguka kwa vipando vyao, mkusanyiko wa maadui
6Hakika binadamu ni mkanushaji sana neema za Mola wake
7Na yeye anakubali ukanushaji wake
8Na yeye ana pupa sana la mali
9Kwani binadamu hajui linalomngojea mbele yake, pindi Mwenyezi Mungu Atakapowatoa wafu makaburini waende kuhesabiwa na kulipwa
10Na (kwani yeye hajui) yakatolewa yaliyo ndani ya vifua: mema au maovu
11Hakika Mola wao kwao na kwa amali zao, Siku Hiyo, ni Mtambuzi; hakuna chenye kufichamana Kwake
chanzo: Abdullah Muhammad Abu Bakr
WEBREATH · 11:11
«If you are thankful, I will give you more» — Quran 14:7
Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.
WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath