Ukristo
nyuma

Zaburi 9

1Ee Bwana, nitakutukuza kwa moyo wangu wote, nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu.

2Nitafurahi na kushangilia ndani yako. Nitaliimbia sifa jina lako, Ewe Uliye Juu Sana.

3Adui zangu wamerudi nyuma, wamejikwaa na kuangamia mbele zako.

4Kwa maana umetetea haki yangu na msimamo wangu; umeketi kwenye kiti chako cha enzi, ukihukumu kwa haki.

5Umekemea mataifa na kuwaangamiza waovu; umeyafuta majina yao milele na milele.

6Uharibifu usiokoma umempata adui, umeingʼoa miji yao; hata kumbukumbu lao limetoweka.

7Bwana anatawala milele, ameweka kiti chake cha enzi apate kuhukumu.

8Mungu atahukumu ulimwengu kwa haki, atatawala mataifa kwa haki.

9Bwana ni kimbilio la watu wanaoonewa, ni ngome imara wakati wa shida.

10Wote wanaolijua jina lako watakutumaini wewe, kwa maana wewe Bwana, hujawaacha kamwe wakutafutao.

11Mwimbieni Bwana sifa, amefanywa mtawala Sayuni, tangazeni miongoni mwa mataifa, yale aliyoyatenda.

12Kwa maana yeye alipizaye kisasi cha damu hukumbuka, hapuuzi kilio cha wanaoonewa.

13Ee Bwana, tazama jinsi walivyo wengi adui zangu wanaonitesa! Nihurumie, uniinue kutoka malango ya mauti,

14ili niweze kutangaza sifa zako katika malango ya Binti Sayuni na huko niushangilie wokovu wako.

15Mataifa wameanguka kwenye shimo walilolichimba, miguu yao imenaswa kwenye wavu waliouficha.

16Bwana anajulikana kwa haki yake, waovu wamenaswa katika kazi za mikono yao.

17Waovu wataishia kuzimu, naam, mataifa yote wanaomsahau Mungu.

18Lakini mhitaji hatasahaulika siku zote, wala matumaini ya walioonewa hayatapotea.

19Ee Bwana, inuka, usimwache binadamu ashinde. Mataifa na yahukumiwe mbele zako.

20Ee Bwana, wapige kwa hofu, mataifa na yajue kuwa wao ni watu tu.

chanzo: Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™

WEBREATH · 11:11

«He himself gives everyone life and breath and everything else» — Acts 17:25

Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.

WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath