Zaburi 97
1Bwana anatawala, nchi na ifurahi, visiwa vyote vishangilie.
2Mawingu na giza nene vinamzunguka, haki na hukumu ndio msingi wa kiti chake cha enzi.
3Moto hutangulia mbele zake na huteketeza adui zake pande zote.
4Umeme wake wa radi humulika dunia, nchi huona na kutetemeka.
5Milima huyeyuka kama nta mbele za Bwana, mbele za Bwana wa dunia yote.
6Mbingu zinatangaza haki yake, na mataifa yote huona utukufu wake.
7Wote waabuduo sanamu waaibishwa, wale wajisifiao sanamu: mwabuduni yeye, enyi miungu yote!
8Sayuni husikia na kushangilia, vijiji vya Yuda vinafurahi kwa sababu ya hukumu zako, Ee Bwana.
9Kwa kuwa wewe, Ee Bwana, ndiwe Uliye Juu Sana kuliko dunia yote; umetukuka sana juu ya miungu yote.
10Wale wanaompenda Bwana na wauchukie uovu, kwa maana yeye hulinda maisha ya waaminifu wake na kuwaokoa kutoka mkononi mwa mwovu.
11Nuru huangaza wenye haki na furaha kwa watu wanyofu wa moyo.
12Furahini katika Bwana, ninyi mlio wenye haki, lisifuni jina lake takatifu.
WEBREATH · 11:11
«He himself gives everyone life and breath and everything else» — Acts 17:25
Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.
WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath