Ukristo
nyuma

Zaburi 85

1Ee Bwana, ulionyesha wema kwa nchi yako. Ulimrejeshea Yakobo baraka zake.

2Ulisamehe uovu wa watu wako, na kufunika dhambi zao zote.

3Uliweka kando ghadhabu yako yote na umegeuka na kuiacha hasira yako kali.

4Ee Mungu Mwokozi wetu, uturejeshe tena, nawe uiondoe chuki yako juu yetu.

5Je, utatukasirikia milele? Utaendeleza hasira yako kwa vizazi vyote?

6Je, hutatuhuisha tena, ili watu wako wakufurahie?

7Utuonyeshe upendo wako usiokoma, Ee Bwana, utupe wokovu wako.

8Nitasikiliza lile atakalosema Mungu aliye Bwana; anaahidi amani kwa watu wake, watakatifu wake: lakini nao wasirudie upumbavu.

9Hakika wokovu wake uko karibu na wale wamchao, ili utukufu wake udumu katika nchi yetu.

10Upendo na uaminifu hukutana pamoja, haki na amani hubusiana.

11Uaminifu huchipua kutoka nchi, haki hutazama chini kutoka mbinguni.

12Naam, hakika Bwana atatoa kilicho chema, nayo nchi yetu itazaa mavuno yake.

13Haki itatangulia mbele yake na kutengeneza njia kwa ajili ya hatua zake.

chanzo: Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™

WEBREATH · 11:11

«He himself gives everyone life and breath and everything else» — Acts 17:25

Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.

WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath