Ukristo
nyuma

Zaburi 83

1Ee Mungu, usinyamaze kimya, usinyamaze, Ee Mungu, usitulie.

2Tazama watesi wako wanafanya fujo, jinsi adui zako wanavyoinua vichwa vyao.

3Kwa hila, wanafanya shauri dhidi ya watu wako, wanafanya shauri baya dhidi ya wale unaowapenda.

4Wanasema, “Njooni, tuwaangamize kama taifa, ili jina la Israeli lisikumbukwe tena.”

5Kwa nia moja wanapanga mashauri mabaya pamoja, wanafanya muungano dhidi yako,

6mahema ya Edomu na Waishmaeli, ya Wamoabu na Wahagari,

7Gebali, Amoni na Amaleki, Ufilisti, pamoja na watu wa Tiro.

8Hata Ashuru wameungana nao kuwapa nguvu wazao wa Loti.

9Uwatendee kama vile ulivyowatendea Midiani, na kama vile ulivyowatendea Sisera na Yabini hapo kijito cha Kishoni,

10ambao waliangamia huko Endori na wakawa kama takataka juu ya nchi.

11Wafanye wakuu wao kama Orebu na Zeebu, watawala wao kama Zeba na Salmuna,

12ambao walisema, “Na tumiliki nchi ya malisho ya Mungu.”

13Ee Mungu wangu, wapeperushe kama mavumbi ya kisulisuli, kama makapi yapeperushwayo na upepo.

14Kama vile moto uteketezavyo msitu au mwali wa moto unavyounguza milima,

15wafuatilie kwa tufani yako na kuwafadhaisha kwa dhoruba yako.

16Funika nyuso zao kwa aibu ili watu walitafute jina lako, Ee Bwana.

17Wao na waaibishwe na kufadhaishwa milele, na waangamie kwa aibu.

18Hebu wajue kwamba wewe, ambaye jina lako ni Bwana, kwamba wewe peke yako ndiwe Uliye Juu Sana ya dunia yote.

chanzo: Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™

WEBREATH · 11:11

«He himself gives everyone life and breath and everything else» — Acts 17:25

Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.

WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath