Zaburi 72
1Ee Mungu, mjalie mfalme aamue kwa haki yako, mwana wa mfalme kwa haki yako.
2Atawaamua watu wako kwa haki, watu wako walioonewa kwa haki.
3Milima italeta mafanikio kwa watu, vilima tunda la haki.
4Atawatetea walioonewa miongoni mwa watu na atawaokoa watoto wa wahitaji, ataponda mdhalimu.
5Atadumu kama jua lidumuvyo, kama mwezi, vizazi vyote.
6Atakuwa kama mvua inyeshayo juu ya shamba lililofyekwa, kama manyunyu yanyeshayo ardhi.
7Katika siku zake wenye haki watastawi; mafanikio yatakuwepo mpaka mwezi utakapokoma.
8Atatawala kutoka bahari hadi bahari na kutoka Mto mpaka miisho ya dunia.
9Makabila ya jangwani watamsujudia, na adui zake wataramba mavumbi.
10Wafalme wa Tarshishi na wa pwani za mbali watamletea kodi; wafalme wa Sheba na Seba watampa zawadi.
11Wafalme wote watamsujudia na mataifa yote yatamtumikia.
12Kwa maana atamwokoa mhitaji anayemlilia, aliyeonewa asiye na wa kumsaidia.
13Atawahurumia wanyonge na wahitaji na kuwaokoa wahitaji kutoka mauti.
14Atawaokoa kutoka uonevu na ukatili, kwani damu yao ni ya thamani machoni pake.
15Aishi maisha marefu! Na apewe dhahabu ya Sheba. Watu wamwombee daima na kumbariki mchana kutwa.
16Nafaka ijae tele katika nchi yote, juu ya vilele vya vilima na istawi. Tunda lake na listawi kama Lebanoni, listawi kama majani ya kondeni.
17Jina lake na lidumu milele, na lidumu kama jua. Mataifa yote yatabarikiwa kupitia kwake, nao watamwita aliyebarikiwa.
18Bwana Mungu, Mungu wa Israeli, apewe sifa, yeye ambaye peke yake hutenda mambo ya ajabu.
19Jina lake tukufu lisifiwe milele, ulimwengu wote ujae utukufu wake. Amen na Amen.
20Huu ndio mwisho wa maombi ya Daudi mwana wa Yese.
WEBREATH · 11:11
«He himself gives everyone life and breath and everything else» — Acts 17:25
Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.
WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath