Ukristo
nyuma

Zaburi 48

1Bwana ni mkuu, anayestahili kusifiwa sana, katika mji wa Mungu wetu, mlima wake mtakatifu.

2Ni mzuri katika kuinuka kwake juu sana, furaha ya dunia yote. Kama vilele vya juu sana vya Safoni ni Mlima Sayuni, mji wa Mfalme Mkuu.

3Mungu yuko katika ngome zake; amejionyesha mwenyewe kuwa ngome yake.

4Wakati wafalme walipounganisha nguvu, waliposonga mbele pamoja,

5walimwona nao wakashangaa, wakakimbia kwa hofu.

6Kutetemeka kuliwashika huko, maumivu kama ya mwanamke mwenye utungu wa kuzaa.

7Uliwaangamiza kama meli za Tarshishi zilizovunjwa na upepo wa mashariki.

8Kama tulivyokuwa tumesikia, ndivyo tulivyoona katika mji wa Bwana Mwenye Nguvu Zote, katika mji wa Mungu wetu: Mungu ataufanya uwe salama milele.

9Ee Mungu, hekaluni mwako tunatafakari upendo wako usiokoma.

10Ee Mungu, kama jina lako lilivyo, sifa zako zinafika hadi miisho ya dunia, mkono wako wa kuume umejazwa na haki.

11Mlima Sayuni unashangilia, vijiji vya Yuda vinafurahi kwa sababu ya hukumu zako.

12Tembeeni katika Sayuni, uzungukeni mji, hesabuni minara yake;

13yatafakarini vyema maboma yake, angalieni ngome zake, ili mpate kusimulia habari zake kwa kizazi kijacho.

14Kwa kuwa huyu Mungu ni Mungu wetu milele na milele; atakuwa kiongozi wetu hata mwisho.

chanzo: Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™

WEBREATH · 11:11

«He himself gives everyone life and breath and everything else» — Acts 17:25

Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.

WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath