Zaburi 47
1Pigeni makofi, enyi mataifa yote, mpigieni Mungu kelele za shangwe!
2Jinsi gani alivyo wa kutisha, Bwana Aliye Juu Sana, Mfalme mkuu juu ya dunia yote!
3Ametiisha mataifa chini yetu watu wengi chini ya miguu yetu.
4Alituchagulia urithi wetu, fahari ya Yakobo, aliyempenda.
5Mungu amepaa kwa kelele za shangwe, Bwana kwa sauti za tarumbeta.
6Mwimbieni Mungu sifa, imbeni sifa, mwimbieni sifa Mfalme wetu, imbeni sifa.
7Kwa kuwa Mungu ni mfalme wa dunia yote, mwimbieni zaburi za sifa.
8Mungu anatawala juu ya mataifa, Mungu ameketi juu ya kiti chake cha enzi kitakatifu.
9Wakuu wa mataifa wanakusanyika kama watu wa Mungu wa Abrahamu, kwa kuwa wafalme wa dunia ni mali ya Mungu; yeye ametukuka sana.
WEBREATH · 11:11
«He himself gives everyone life and breath and everything else» — Acts 17:25
Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.
WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath