Ukristo
nyuma

Zaburi 41

1Heri mtu yule anayemjali mnyonge, Bwana atamwokoa wakati wa shida.

2Bwana atamlinda na kuyahifadhi maisha yake, atambariki katika nchi na hatamwacha katika tamaa ya adui zake.

3Bwana atamtegemeza awapo mgonjwa kitandani, atamwinua kutoka kitandani mwake.

4Nilisema, “Ee Bwana nihurumie, niponye, maana nimekutenda dhambi wewe.”

5Adui zangu wanasema kwa hila, “Lini atakufa, na jina lake litokomee kabisa.”

6Kila anapokuja mtu kunitazama, huzungumza uongo, huku moyo wake hukusanya masingizio; kisha huondoka na kuyasambaza huku na huko.

7Adui zangu wote hunongʼonezana dhidi yangu, hao huniwazia mabaya sana, wakisema,

8“Ugonjwa mbaya sana umempata, kamwe hatainuka tena kitandani mwake.”

9Hata rafiki yangu wa karibu niliyemwamini, yule aliyekula chakula changu ameniinulia kisigino chake.

10Lakini wewe, Ee Bwana, nihurumie, ukaniinue tena, ili niweze kuwalipiza kisasi.

11Najua kwamba wapendezwa nami, kwa kuwa adui yangu hanishindi.

12Katika uadilifu wangu unanitegemeza na kuniweka kwenye uwepo wako milele.

13Msifuni Bwana, Mungu wa Israeli, tangu milele na hata milele. Amen na Amen.

chanzo: Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™

WEBREATH · 11:11

«He himself gives everyone life and breath and everything else» — Acts 17:25

Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.

WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath