Zaburi 3
1Ee Bwana, tazama adui zangu walivyo wengi! Ni wengi kiasi gani wanaoinuka dhidi yangu!
2Wengi wanasema juu yangu, “Mungu hatamwokoa.”
3Lakini wewe, Ee Bwana, ni ngao pande zote; umeniwekea utukufu na kuinua kichwa changu.
4Ninamlilia Bwana kwa sauti kuu, naye ananijibu kutoka mlima wake mtakatifu.
5Ninajilaza na kupata usingizi; naamka tena, kwa maana Bwana hunitegemeza.
6Sitaogopa makumi elfu ya adui, wanaojipanga dhidi yangu kila upande.
7Ee Bwana, amka! Niokoe, Ee Mungu wangu! Wapige adui zangu wote kwenye taya, vunja meno ya waovu.
8Kwa maana wokovu watoka kwa Bwana. Baraka yako na iwe juu ya watu wako.
WEBREATH · 11:11
«He himself gives everyone life and breath and everything else» — Acts 17:25
Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.
WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath