Ukristo
nyuma

Zaburi 30

1Nitakutukuza wewe, Ee Bwana, kwa kuwa umeniinua kutoka vilindi, na hukuacha adui zangu washangilie juu yangu.

2Ee Bwana, Mungu wangu, nilikuita unisaidie na wewe umeniponya.

3Ee Bwana, umenitoa Kuzimu, umeniokoa nisishuke kwenye shimo la mauti.

4Mwimbieni Bwana, enyi watakatifu wake; lisifuni jina lake takatifu.

5Kwa maana hasira yake ni ya muda mfupi, bali upendo wake hudumu siku zote. Inawezekana kilio kiwepo usiku kucha, lakini asubuhi kukawa na furaha.

6Nilipofanikiwa nilisema, “Sitatikiswa kamwe.”

7Ee Bwana, uliponijalia, uliuimarisha mlima wangu, lakini ulipouficha uso wako nilifadhaika.

8Kwako wewe, Ee Bwana, niliita, kwa Bwana niliomba rehema:

9“Kuna faida gani katika kuangamia kwangu? Katika kushuka kwangu shimoni? Je, mavumbi yatakusifu? Je, yatatangaza uaminifu wako?

10Ee Bwana, unisikie na kunihurumia, Ee Bwana, uwe msaada wangu.”

11Uligeuza maombolezo yangu kuwa kucheza, ulinivua nguo za gunia ukanivika shangwe,

12ili moyo wangu uweze kukusifu na usikae kimya. Ee Bwana Mungu wangu, nitakushukuru milele.

chanzo: Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™

WEBREATH · 11:11

«He himself gives everyone life and breath and everything else» — Acts 17:25

Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.

WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath