Zaburi 2
1Kwa nini mataifa wanashauriana kufanya mabaya, na kabila za watu kula njama bure?
2Wafalme wa dunia wanajipanga na watawala wanajikusanya pamoja dhidi ya Bwana na dhidi ya Mpakwa Mafuta wake.
3Wanasema, “Tuvunje minyororo yao na kuvitupilia mbali vifungo vyao.”
4Yeye atawalaye mbinguni hucheka, Bwana huwadharau.
5Kisha huwakemea katika hasira yake na kuwaogopesha katika ghadhabu yake, akisema,
6“Nimemtawaza Mfalme wangu juu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu.”
7Nitatangaza amri ya Bwana: Yeye aliniambia, “Wewe ni Mwanangu, leo mimi nimekuzaa.
8Niombe, nami nitayafanya mataifa kuwa urithi wako, miisho ya dunia kuwa milki yako.
9Utawatawala kwa fimbo ya chuma na kuwavunjavunja kama chombo cha mfinyanzi.”
10Kwa hiyo, ninyi wafalme, kuweni na hekima; mwonyeke, enyi watawala wa dunia.
11Mtumikieni Bwana kwa hofu na mshangilie kwa kutetemeka.
12Mbusu Mwana, asije akakasirika nawe ukaangamizwa katika njia yako, kwa maana hasira yake inaweza kuwaka ghafula. Heri wote wanaomkimbilia.
WEBREATH · 11:11
«He himself gives everyone life and breath and everything else» — Acts 17:25
Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.
WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath