Zaburi 20
1Bwana na akujibu unapokuwa katika dhiki, jina la Mungu wa Yakobo na liwe kinga yako.
2Na akutumie msaada kutoka patakatifu na akupatie msaada kutoka Sayuni.
3Na azikumbuke dhabihu zako zote, na azikubali sadaka zako za kuteketezwa.
4Na akujalie haja ya moyo wako, na aifanikishe mipango yako yote.
5Tutashangilia kwa furaha utakaposhinda, tutainua bendera zetu kwa jina la Mungu wetu. Bwana na akupe haja zako zote.
6Sasa nafahamu kuwa Bwana humwokoa mpakwa mafuta wake, humjibu kutoka mbingu yake takatifu kwa nguvu za wokovu wa mkono wake wa kuume.
7Wengine wanatumaini magari ya vita, na wengine farasi, bali sisi tutalitumainia jina la Bwana, Mungu wetu.
8Wao wameshushwa chini na kuanguka, bali sisi tunainuka na kusimama imara.
9Ee Bwana, mwokoe mfalme! Tujibu tunapokuita!
WEBREATH · 11:11
«He himself gives everyone life and breath and everything else» — Acts 17:25
Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.
WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath