Ukristo
nyuma

Zaburi 17

1Sikia, Ee Bwana, kusihi kwangu kwa haki, sikiliza kilio changu. Tega sikio kwa ombi langu, halitoki kwenye midomo ya udanganyifu.

2Hukumu yangu na itoke kwako, macho yako na yaone yale yaliyo haki.

3Ingawa unauchunguza moyo wangu na kunikagua usiku, ingawa umenijaribu, hutaona chochote. Nimeamua kwamba kinywa changu hakitatenda dhambi.

4Kuhusu matendo ya wanadamu: kwa neno la midomo yako, nimejiepusha na njia za wenye jeuri.

5Hatua zangu zimeshikamana na njia zako; nyayo zangu hazikuteleza.

6Ee Mungu, ninakuita, kwa kuwa utanijibu, nitegee sikio lako na usikie ombi langu.

7Uonyeshe ajabu ya upendo wako mkuu, wewe uokoaye kwa mkono wako wa kuume wale wanaokukimbilia kutokana na adui zao.

8Nilinde kama mboni ya jicho lako, unifiche chini ya kivuli cha mbawa zako

9kutokana na waovu wanaonishambulia, kutokana na adui wauaji wanaonizunguka.

10Huifunga mioyo yao iliyo migumu, vinywa vyao hunena kwa majivuno.

11Wamenifuatia nyayo zangu, sasa wamenizingira, wakiwa macho, waniangushe chini.

12Wamefanana na simba mwenye njaa awindaye, kama simba mkubwa anyemeleaye mafichoni.

13Inuka, Ee Bwana, pambana nao, uwaangushe, niokoe kutokana na waovu kwa upanga wako.

14Ee Bwana, mkono wako uniokoe na watu wa jinsi hii, kutokana na watu wa ulimwengu huu ambao fungu lao liko katika maisha haya. Na wapate adhabu ya kuwatosha. Watoto wao na wapate zaidi ya hayo, hukumu na iendelee kwa watoto wa watoto wao.

15Na mimi katika haki nitauona uso wako, niamkapo, nitaridhika kwa kuona sura yako.

chanzo: Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™

WEBREATH · 11:11

«He himself gives everyone life and breath and everything else» — Acts 17:25

Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.

WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath