Zaburi 16
1Ee Mungu, uniweke salama, kwa maana kwako nimekimbilia.
2Nilimwambia Bwana, “Wewe ndiwe Bwana wangu; pasipo wewe sina jambo jema.”
3Kwa habari ya watakatifu walioko duniani, ndio walio wa fahari ambao ninapendezwa nao.
4Huzuni itaongezeka kwa wale wanaokimbilia miungu mingine. Sitazimimina sadaka zao za damu au kutaja majina yao midomoni mwangu.
5Bwana umeniwekea fungu langu na kikombe changu; umeyafanya mambo yangu yote yawe salama.
6Alama za mipaka zimeniangukia mahali pazuri, hakika nimepata urithi mzuri.
7Nitamsifu Bwana ambaye hunishauri, hata wakati wa usiku moyo wangu hunifundisha.
8Nimemweka Bwana mbele yangu daima. Kwa sababu yuko mkono wangu wa kuume, sitatikisika.
9Kwa hiyo moyo wangu unafurahia, na ulimi wangu unashangilia; mwili wangu nao utapumzika salama,
10kwa maana hutaniacha kaburini, wala hutamwacha Mtakatifu Wako kuona uharibifu.
11Umenijulisha njia ya uzima; utanijaza na furaha mbele zako, pamoja na furaha za milele katika mkono wako wa kuume.
WEBREATH · 11:11
«He himself gives everyone life and breath and everything else» — Acts 17:25
Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.
WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath