Ukristo
nyuma

Zaburi 149

1Msifuni Bwana. Mwimbieni Bwana wimbo mpya, sifa zake katika kusanyiko la watakatifu.

2Israeli na washangilie katika Muumba wao, watu wa Sayuni na wafurahi katika Mfalme wao.

3Na walisifu jina lake kwa kucheza na wampigie muziki kwa matari na kinubi.

4Kwa maana Bwana anapendezwa na watu wake, anawavika wanyenyekevu taji ya wokovu.

5Watakatifu washangilie katika heshima hii, na waimbe kwa shangwe vitandani mwao.

6Sifa za Mungu na ziwe vinywani mwao na upanga ukatao kuwili mikononi mwao,

7ili walipize mataifa kisasi na adhabu juu ya mataifa,

8wawafunge wafalme wao kwa minyororo, wakuu wao kwa pingu za chuma,

9ili kuwafanyia hukumu iliyoandikwa dhidi yao. Huu ndio utukufu wa watakatifu wake wote. Msifuni Bwana.

chanzo: Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™

WEBREATH · 11:11

«He himself gives everyone life and breath and everything else» — Acts 17:25

Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.

WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath