Ukristo
nyuma

Zaburi 122

1Nilishangilia pamoja na wale walioniambia, “Twende nyumbani ya Bwana.”

2Ee Yerusalemu, miguu yetu imesimama malangoni mwako.

3Yerusalemu imejengwa vyema kama mji ambao umeshikamanishwa pamoja.

4Huko ndiko makabila hukwea, makabila ya Bwana, kulisifu jina la Bwana kulingana na maagizo waliopewa Israeli.

5Huko viti vya enzi vya hukumu hukaa, viti vya enzi vya nyumba ya Daudi.

6Omba kwa ajili ya amani ya Yerusalemu: “Wote wakupendao na wawe salama.

7Amani na iwepo ndani ya kuta zako na usalama ndani ya ngome zako.”

8Kwa ajili ya ndugu zangu na marafiki, nitasema, “Amani iwe ndani yako.”

9Kwa ajili ya nyumba ya Bwana Mungu wetu, nitatafuta mafanikio yako.

chanzo: Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™

WEBREATH · 11:11

«He himself gives everyone life and breath and everything else» — Acts 17:25

Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.

WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath