Zaburi 120
1Katika dhiki yangu namwita Bwana, naye hunijibu.
2Ee Bwana, uniokoe kutoka midomo ya uongo na ndimi za udanganyifu.
3Atakufanyia nini, au akufanyie nini zaidi, ewe ulimi mdanganyifu?
4Atakuadhibu kwa mishale mikali ya shujaa, kwa makaa yanayowaka ya mti wa mretemu.
5Ole wangu kwa kuwa naishi Mesheki, kwamba naishi katikati ya hema za Kedari!
6Nimeishi muda mrefu mno miongoni mwa wale wanaochukia amani.
7Mimi ni mtu wa amani; lakini ninaposema, wao wanataka vita.
WEBREATH · 11:11
«He himself gives everyone life and breath and everything else» — Acts 17:25
Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.
WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath