Zaburi 113
1Msifuni Bwana. Enyi watumishi wa Bwana msifuni, lisifuni jina la Bwana.
2Jina la Bwana na lisifiwe, sasa na hata milele.
3Kuanzia mawio ya jua hadi machweo yake, jina la Bwana linapaswa kusifiwa.
4Bwana ametukuka juu ya mataifa yote, utukufu wake juu ya mbingu.
5Ni nani aliye kama Bwana Mungu wetu, Yeye ambaye ameketi juu kwenye kiti cha enzi,
6ambaye huinama atazame chini aone mbingu na nchi?
7Huwainua maskini kutoka mavumbini, na kuwanyanyua wahitaji kutoka kwenye jalala,
8huwaketisha pamoja na wakuu, pamoja na wakuu wa watu wake.
9Humjalia mwanamke tasa kutulia nyumbani mwake, akiwa mama watoto mwenye furaha. Msifuni Bwana.
WEBREATH · 11:11
«He himself gives everyone life and breath and everything else» — Acts 17:25
Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.
WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath