Zaburi 111
1Msifuni Bwana. Nitamtukuza Bwana kwa moyo wangu wote, katika baraza la wanyofu na katika kusanyiko.
2Kazi za Bwana ni kuu, wote wanaopendezwa nazo huzitafakari.
3Kazi zake zimejaa fahari na utukufu, haki yake hudumu daima.
4Amefanya maajabu yake yakumbukwe, Bwana ni mwenye neema na huruma.
5Huwapa chakula wale wanaomcha, hulikumbuka agano lake milele.
6Amewaonyesha watu wake uwezo wa kazi zake, akiwapa nchi za mataifa mengine.
7Kazi za mikono yake ni za uaminifu na haki, mausia yake yote ni ya kuaminika.
8Zinadumu milele na milele, zikifanyika kwa uaminifu na unyofu.
9Aliwapa watu wake ukombozi, aliamuru agano lake milele: jina lake ni takatifu na la kuogopwa.
10Kumcha Bwana ndicho chanzo cha hekima, wote wanaozifuata amri zake wana busara. Sifa zake zadumu milele.
WEBREATH · 11:11
«He himself gives everyone life and breath and everything else» — Acts 17:25
Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.
WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath