Zaburi 108
1Ee Mungu, moyo wangu ni thabiti; nitaimba na kusifu kwa moyo wangu wote.
2Amka, kinubi na zeze! Nitayaamsha mapambazuko.
3Nitakusifu wewe, Ee Bwana, katikati ya mataifa; nitaimba habari zako, katikati ya jamaa za watu.
4Kwa maana upendo wako ni mkuu, ni juu kuliko mbingu; uaminifu wako unazifikia anga.
5Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu, utukufu wako na uenee duniani kote.
6Tuokoe na utusaidie kwa mkono wako wa kuume, ili wale uwapendao wapate kuokolewa.
7Mungu amenena kutoka patakatifu pake: “Nitaigawa Shekemu kwa ushindi na kulipima Bonde la Sukothi.
8Gileadi ni yangu, Manase ni yangu, Efraimu ni kofia yangu ya chuma, nayo Yuda ni fimbo yangu ya utawala.
9Moabu ni sinia langu la kunawia, juu ya Edomu natupa kiatu changu; nashangilia kwa kushindwa kwa Ufilisti.”
10Ni nani atakayenipeleka hadi mji wenye ngome? Ni nani atakayeniongoza hadi nifike Edomu?
11Ee Mungu, si ni wewe uliyetukataa sisi, na hutoki tena na majeshi yetu?
12Tuletee msaada dhidi ya adui, kwa maana msaada wa mwanadamu haufai kitu.
13Kwa msaada wa Mungu tutapata ushindi, naye atawaponda adui zetu.
WEBREATH · 11:11
«He himself gives everyone life and breath and everything else» — Acts 17:25
Breath is one for all: everyone lives by it, whoever they are and whatever they believe. Every day at 11:11 local time people stop for sixty seconds, breathe, and thank GOD for the breath — each in their own words, each within themselves. In that minute we are One Breath.
WEBREATH — the Minute at 11:11, your own local time — we are One Breath